Majina ya waliopata Mkopo HESLB Awamu ya Nne 2021/22
HomeHabari

Majina ya waliopata Mkopo HESLB Awamu ya Nne 2021/22

 Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) jana (Ijumaa, Oktoba 29, 2021) imetangaza Orodha ya Nne yenye wanafunzi wapya 5,003 w...

Kichwa cha Treni Chaibua Mjadala, Serikali Yafafanua
Mwenyekiti Baraza la Chadema afutiwa kesi, akamatwa tena
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo February 23

 Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) jana (Ijumaa, Oktoba 29, 2021) imetangaza Orodha ya Nne yenye wanafunzi wapya 5,003 wa mwaka wa kwanza waliopangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 11.6 bilioni.

Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Abdul-Razaq Badru amewaeleza wanahabari jijini Dar es salaam kuwa baada ya kutangazwa kwa orodha hiyo, jumla ya wanufaika wa mwaka wa kwanza sasa imefikia 65,359 ambao wamepangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 168.9 bilioni.


👉Kutazama majina ya Waliopata Mkopo awamu ya nne <<BOFYA HAPA>>

 “Orodha hii ya nne ina wanufaika 5,003 ambao muda wowote kuanzia sasa wanaweza kuingia katika akaunti zao za SIPA walizoombea mkopo na kupata taarifa zaidi,” amesema Badru katika mkutano na wanahabari uliofanyika katika ofisi za HESLB jijini Dar es salaam.

Akifafanua zaidi kuhusu wanufaika hao 65,359, Badru amesema wanufaika 1,133 ni yatima waliofiwa wazazi wawili; 9,450 waliofiwa na mzazi mmoja; 198 ni wanafunzi wenye ulemavu; 2,919 walifadhiliwa na taasisi mbalimbali katika masomo yao ya sekondari; na 51,559 wanatoka katika kaya masikini.

👉Kutazama majina ya Waliopata Mkopo awamu ya nne <<BOFYA HAPA>>

 “Kwa takwimu hizi, mtaona kuwa ile dhamira ya Serikali kuwawezesha vijana kutoka kaya masikini inathibitika,” amesema Badru na kuongeza kuwa asilimia 41 ya wanufaika 65,359 ni wanawake na asilimia 59 ni wanaume.

Mikopo kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo

Wakati huohuo, Badru amesema kuwa HESLB inakamilisha malipo ya wanafunzi 74,440 ambao ni wanufaika wanaoendelea na masomo baada ya kupokea matokeo yao ya mitihani yanayothibitisha kuwa wamefaulu kuendelea na masomo.

“Tuna wanufaika zaidi ya 98,000 wanaoendelea na masomo na hadi leo (Ijumaa, Oktoba 29, 2021) tumeshapokea matokeo ya mitihani ya wanafunzi 74,440 waliofaulu na tutaanza kutuma fedha kesho,” amesema Badru na kuvikumbusha vyuo kuwasilisha matokeo ya wanufaika waliobaki.

Dirisha la Rufaa

👉Kutazama majina ya Waliopata Mkopo awamu ya nne <<BOFYA HAPA>>

 Kuhusu hatua inayofuata, Badru amesema dirisha la rufaa litafunguliwa Novemba 6, 2021 ili kuwapa fursa wanafunzi ambao hawajaridhika na viwango vya mikopo vya sasa kuwasilisha maombi ya kuongezewa.

Wanaoendelea na masomo na wameomba mkopo kwa 2021/2022

“Tumekua tukipokea maswali kuhusu wanafunzi wanaoendelea na masomo ambao wameomba mkopo mwaka huu … tunakamilisha orodha yao na tutaitoa siku chache zijazo baada ya kujiridhisha na uhitaji wao na kuthibitisha kuwa wamefaulu mitihani yao na matokeo yao yamewasilishwa kwetu,” amefafanua Badru.

Elimu kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza

Katika hatua nyingine, Badru amesema maafisa wa HESLB wanaendelea na mikutano na wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliopo vyuoni ili kuwaelimisha kuhusu taratibu za malipo na kufafanua masuala mbalimbali yanayojitokeza.

👉Kutazama majina ya Waliopata Mkopo awamu ya nne <<BOFYA HAPA>>



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Majina ya waliopata Mkopo HESLB Awamu ya Nne 2021/22
Majina ya waliopata Mkopo HESLB Awamu ya Nne 2021/22
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEinyfVHJ9bNKkvnjRaSHznQANd0ov37TXY5M02wR4POZT_xXZQsZgiVbPcAwd4bjLucebvn3fXcPzKL-Wa71pLGuQ-WHucHCjLQB_ZIcvvnBF8q7CA2OBkr15coNNhZpoVw5flVniDeeTxKFrAtD0UtkEjbnan24YTaltrQcGPZdewYHnr36Zkkf_16NQ=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEinyfVHJ9bNKkvnjRaSHznQANd0ov37TXY5M02wR4POZT_xXZQsZgiVbPcAwd4bjLucebvn3fXcPzKL-Wa71pLGuQ-WHucHCjLQB_ZIcvvnBF8q7CA2OBkr15coNNhZpoVw5flVniDeeTxKFrAtD0UtkEjbnan24YTaltrQcGPZdewYHnr36Zkkf_16NQ=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/10/majina-ya-waliopata-mkopo-heslb-awamu.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/10/majina-ya-waliopata-mkopo-heslb-awamu.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy