Wataalamu Nishati Wapewa Maagizo Mradi Wa EACOP
HomeHabari

Wataalamu Nishati Wapewa Maagizo Mradi Wa EACOP

Na Dorina G. Makaya & Janeth Mesomapya Waziri wa Nishati, Mh. January Yusuf Makamba, amewaagiza wataalamu wa Wizara ya Nishati kuunda...

Dkt.Ndumbaro Ataja Manufaa Ya Fedha Za Mkopo Kwa Wananchi Wa Mkoa Wa Ruvuma
CCM Wasema Yanayofanywa Na Rais Samia Yanabaraka Zote Za Chama
Spika Ndugai Atoa Ufafanuzi Kuhusu Hotuba Yake Iliyozua Taharuki

Na Dorina G. Makaya & Janeth Mesomapya
Waziri wa Nishati, Mh. January Yusuf Makamba, amewaagiza wataalamu wa Wizara ya Nishati kuunda timu itakayojumuisha sekretarieti za mikoa minane ambapo utapita mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) ili kutengeneza maelezo mahususi ya mikoa hiyo yatakayofanikisha unufaikaji wa fursa zitokanazo na utekelezaji wa mradi huo.

Waziri Makamba ameyasema hayo  Septemba 28, 2021 katika siku ya pili ya semina kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa mikoa hiyo inayoendelea jijini Tanga. Semina hiyo ina lengo la kubainisha fursa zitokanazo na mradi huo wa bomba la mafuta.

Ameelekeza kuwa maelezo hayo mahususi yatoe taarifa kamili kuhusu mahitaji kwenye mikoa hiyo katika kipindi chote cha utekelezaji wa mradi, maandalizi wanayotakiwa kuyafanya ili kukidhi mahitaji husika, thamani ya kazi kiuchumi, na mchanganuo wa fursa zitakazopatikana kulingana na mikoa hiyo na jiografia zake.

“Baada ya kupatikana maelezo hayo, iangaliwe namna bora ya kuwajengea uwezo wananchi wa mikoa husika ili wawe na uwezo wa kufanya kazi na kunufaika na fursa hizo, lengo likiwa kuwapa taarifa sahihi juu ya fursa za mradi ili wawe na mategemeo halisia” aliongeza.

Aidha, Waziri Makamba amewaagiza wasimamizi wa mradi huo, kuhakikisha Mpango wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) unalenga kunufaisha jamii zinazozunguka mradi ili manufaa halisi yaonekane pindi mradi unapofikia ukomo.

Kwa upande wa kanzidata maalumu ya watoa huduma inayoendeshwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Waziri Makamba ameagiza kuwa,  ufahamu wa kutosha utolewe kwa wananchi wa jinsi ya kujisajili kwenye kanzidata hiyo, ili watoa huduma wengi zaidi wawe sehemu ya jukwaa hilo.

Naye Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato ameeleza kuwa, ili fursa za mradi huu zinufaishe kwanza jamii zinazopitiwa na bomba, serikali inaandaa mikakati ya kuhakikisha fursa hizo zinabaki ndani ya mikoa husika na kunufaisha watu wake.

“Tutaenda pia kwenye mikoa husika kuwaelezea wananchi fursa zilizopo kwenye mikoa yao kwa mchanganuo mzuri, ili wajiandae kuzichangamkia,” aliongeza. Naibu Waziri Byabato.

Semina hiyo ya siku tatu itamalizika leo.



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Wataalamu Nishati Wapewa Maagizo Mradi Wa EACOP
Wataalamu Nishati Wapewa Maagizo Mradi Wa EACOP
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEja6qEwAb5Z8T1OfZxK_cy9LG2addNKE7r40TOkKwgu25C-ETgytmNUWWrMCYWSjt_FAdgBi2SNxbv9j_y1sQsGqDIb3tNX_PPkCl7hRj8Br6n5esMgMBiHIDVS06vt9EewT7yNwWznzXOz/s16000/1.jpeg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEja6qEwAb5Z8T1OfZxK_cy9LG2addNKE7r40TOkKwgu25C-ETgytmNUWWrMCYWSjt_FAdgBi2SNxbv9j_y1sQsGqDIb3tNX_PPkCl7hRj8Br6n5esMgMBiHIDVS06vt9EewT7yNwWznzXOz/s72-c/1.jpeg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/09/wataalamu-nishati-wapewa-maagizo-mradi.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/09/wataalamu-nishati-wapewa-maagizo-mradi.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy