Dkt.Ndumbaro Ataja Manufaa Ya Fedha Za Mkopo Kwa Wananchi Wa Mkoa Wa Ruvuma
HomeHabari

Dkt.Ndumbaro Ataja Manufaa Ya Fedha Za Mkopo Kwa Wananchi Wa Mkoa Wa Ruvuma

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro amesema  Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma  wana kila sababu ya kumshukuru na kumpongeza Rais...


 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro amesema  Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma  wana kila sababu ya kumshukuru na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ikiwemo kutoa fedha kwenye Wizara ya Maliasili na Utalii za kukarabati miundombinu ya maeneo ya vivutio vya utalii vilivyopo katika Mkoa huo.

Wito huo ameutoa wakati alipoongoza mamia ya wakazi wa Jimbo la Songea mjini kwenda kusheherekea mwaka mpya wa 2022 kwa kufanya utalii wa ndani kwa nyakati tofauti katika Msitu wa Hifadhi ya  Mlima Matogoro pamoja na Bustani ya Wanyamapori ya Ruhila  iliyopo katikati ya   Manispaa ya Songea  Mjini

Akitaja fedha manufaa ya fedha  hizo, Dkt.Ndumbaro amesema Songea ni mji uliobarikiwa kuwa na vivutio vingi vya utalii  hivyo fedha hizo za mkopo zitatumika kwa ajili ya kuimarisha miundombinu ya maeneo ya vivutio ili kuimarisha utalii

Amesisitiza kuwa Hifadhi ya Msitu wa Mlima  Matogoro ni kivutio kikubwa cha utalii katika mkoa huo isipokuwa changamoto ya barabara ndiyo imekuwa kikwazo cha watalii walio wengi kushindwa kufika

Dkt.Ndumbaro amesema kupitia fedha hizo za mkopo itajengwaa barabara ya uhakika itakayofika hadi juu ya misitu ya milima Matogoro ili kuwarahisishia wanaoenda kufanya utalii huku akisisitiza kuwa tayari Mkandarasi amepatikana na anatajiwa kukabidhiwa  eneo la ujenzi tarehe 15 Januari mwaka huu

" Mhe.Rais ametuona na kutuamini  wana Songea kwa kutupatia fedha kwa ajili ya kutengeneza barabara ili kuhakikisha watalii watakaoamua kutumia magari yao kufika katika kilele cha Mlima huo wanaweza kufika tofauti na ilivyosasa magari madogo huku hayawezi kufika kutokana na ubovu wa barabara" alisema Dkt.Ndumbaro

Pia, Dkt.Ndumbaro amesema Mhe.Rais Samia  Samia aliridhia kutengwa kwa bajeti ya mwaka huu ya jumla ya kiasi cha shilingo milioni 50 kwa ajili ya kukarabati uzio wa Bustani ya Wanyamapori ya Ruhila.ambayo imezidi kupata umaarufu siku za hivi karibuni baada ya kufanyika kwa maboresho makubwa

Dkt  Ndumbaro amesema kuboreka kwa miundombinu katika maeneo ya vivutio vya utalii  kutachochea Manispaa ya Songea mjini kimapato.kwa vile Utalii ni sekta mtambuka

 Hata hivyo, Dkt.Ndumbaro amewataka Wakazi wa Songea kuchangamkia fursa za utalii zilizopo katika mkoa huo huku akiwasisitiza kujenga tabia ya kutembelea maeneo ya vivutio hivyo ili kutambua fursa zilizopo kwenye maeneo yao.

Katika hatua nyingine Waziri Ndumbaro  amewataka Wananchi hao kuwa mstari wa mbele kulinda na kuhifadhi maeneo ya vivutio vya utalii badala ya kuiachia Wizara pekee ili maeneo hayo yaweze kuchochea kipato kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla kupitia sekta ya utalii.

Katika kusherehekea sikukuu  ya Mwaka mpya katika Bustani ya Wanyamapori ya Ruhila, Waziri Ndumbaro aliweza kuwalipia wakazi wote wa Songea Mjin i tozo zote za vingilio katika Bustani hiyo pamoja na kuhakikisha  wanakula nyama pori iliyokuwa imeandaliwa kwa ajili ya wakazi hao






Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Dkt.Ndumbaro Ataja Manufaa Ya Fedha Za Mkopo Kwa Wananchi Wa Mkoa Wa Ruvuma
Dkt.Ndumbaro Ataja Manufaa Ya Fedha Za Mkopo Kwa Wananchi Wa Mkoa Wa Ruvuma
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEj2zD82Yls1RQU7mAaGxfxcQjhS593cw6_2OsXrwr7bchVYMczF9QGLGP3VOipW7Pw6WNtGHJzqJnTwaZDf05ANIuRl8S9IoU2QB_9Qg1-CsSkFSU_IEs4ivoch3czUUpARMMFZdm3ZqXlZHkdxcgTgCr4ve-wm9SrrImRFZI6kKJ7xnzFHcx55ht2LhA=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEj2zD82Yls1RQU7mAaGxfxcQjhS593cw6_2OsXrwr7bchVYMczF9QGLGP3VOipW7Pw6WNtGHJzqJnTwaZDf05ANIuRl8S9IoU2QB_9Qg1-CsSkFSU_IEs4ivoch3czUUpARMMFZdm3ZqXlZHkdxcgTgCr4ve-wm9SrrImRFZI6kKJ7xnzFHcx55ht2LhA=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/01/dktndumbaro-ataja-manufaa-ya-fedha-za.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/01/dktndumbaro-ataja-manufaa-ya-fedha-za.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy