UONGOZI wa Simba umewashukuru mashabiki pamoja na wadau ambao walijitokeza jana Septemba 19 kwenye siku ya tamasha ya Simba Day. Tamasha ...
UONGOZI wa Simba umewashukuru mashabiki pamoja na wadau ambao walijitokeza jana Septemba 19 kwenye siku ya tamasha ya Simba Day.
Tamasha hilo ambalo lilikuwa limefana lilihusisha watu wa aina mbalimbali ambapo mashabiki wengi wa mpira walikuwa wanalifuatilia na wale waliokuwa nje ya nchi walikuwa wanalitazama kupitia Azam Tv.
Barbra Gonzalez, Mtendaji Mkuu wa Simba amesema kuwa jambo la furaha kuona namna Wanasimba pamoja na watu wengi walivyojitokeza kwa ajili ya tamasha la Simba Day.
Kifupi tu Barbara amesema:"Asanteni Wanasimba,".
Pia kulikuwa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa ambapo ulipigwa mpira wa kazi kati ya Simba na TP Mazembe baada ya dakika 90, ubao ulisoma Simba 0-1 TP Mazembe.
Ni uzembe wa safu ya ulinzi wa Simba iliyokuwa inaongozwa na Pascal Wawa kufanya makosa ya kushindwa kulinda lango lao jambo ambalo lilisababisha maumivu dakika za jioni.
Erasto Nyoni hakuwa na chaguo alimuacha Baleke Jean dakika ya 84 akifunga bao kwa mtindo wa kubinuka na kuzama mazima nyavuni katika mchezo huo uliohudhiriwa na mashabiki wengi.
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS