Mwenyekiti wa AU ataka Afrika iwe na kiti cha uanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la UN
HomeHabari

Mwenyekiti wa AU ataka Afrika iwe na kiti cha uanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la UN

Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambaye ni mwenyekiti sasa wa Umoja wa Afrika AU amewasilisha malalamiko kadhaa...

China na Belarus zinafanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi karibu na mpaka wa NATO na EU.
Ibrahimovic amethibitisha kuwa Origi amefukuzwa katika timu ya vijana ya AC Milan.
Man Utd itajumuisha kipengele muhimu katika mkataba wa Greenwood wa Marseille.


Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambaye ni mwenyekiti sasa wa Umoja wa Afrika AU amewasilisha malalamiko kadhaa ya bara la Africa katika mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, ulioanza juzi mjini New York, likiwemo la bara la Afrika kupatiwa uanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la UN.

Tshisekedi ambaye ni kiongozi wa kwanza wa nchi za Afrika kuhutubia mkutano wa mwaka huu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, ambao katika ngazi ya juu ya viongozi wa nchi wanachama ulifunguliwa rasmi juzi,  Tshisekedi, amezungumzia Afrika, kwa kuthibitisha mahitaji ya uwakilishi bora wa bara la Afrika kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Mwenyekiti wa AU ameomba nchi mbili za ziada zijumuishwe kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika kundi la nchi wanachama wasio wa kudumu wa baraza hilo; na sambaba na hilo, nchi zingine mbili za Afrika zishiriki kwenye Baraza la Usalama kama wanachama wa kudumu walio na kura ya veto.

Katika hotuba yake hiyo kwa viongozi wanachama wa Umoja wa Mataifa, Rais wa Kongo DR amezungumzia pia vita vya kimataifa dhidi ya ugaidi na akasema: "Afrika imekataa kuwa hifadhi ya ugaidi wa kimataifa".

Mwenyekiti huyo wa mzunguko wa AU, amekosoa uwepo wa makundi yenye misimamo mikali, ambayo amesema yameenea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, baada ya kuenea nchini Mali, Niger, Nigeria, Cameroon, Chad, Burkina Faso na Msumbij.




Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Mwenyekiti wa AU ataka Afrika iwe na kiti cha uanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la UN
Mwenyekiti wa AU ataka Afrika iwe na kiti cha uanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la UN
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjwCAVohJeWy6yiBwDNhKAQ2yGXANmkQ1tbyq0TvKtgh4mluzELmhN-0ipIIH6dCOaYCGv8y7418GEhLvu_JLrXt9KV4Acuf9q2t2D7GpxUNorVWO0u6dWXTXoMFsHLvBgCX85f7bY9Wotd/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjwCAVohJeWy6yiBwDNhKAQ2yGXANmkQ1tbyq0TvKtgh4mluzELmhN-0ipIIH6dCOaYCGv8y7418GEhLvu_JLrXt9KV4Acuf9q2t2D7GpxUNorVWO0u6dWXTXoMFsHLvBgCX85f7bY9Wotd/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/09/mwenyekiti-wa-au-ataka-afrika-iwe-na.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/09/mwenyekiti-wa-au-ataka-afrika-iwe-na.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy