WENGI WANARUDI BONGO WAKITOKA NJE, TATIZO NINI CHIPS AMA KUNA LINGINE?
HomeMichezo

WENGI WANARUDI BONGO WAKITOKA NJE, TATIZO NINI CHIPS AMA KUNA LINGINE?

SASA imekuwa kawaida, tumerudi kulekule kwa mwanzo. Ninawazungumzia wachezaji wetu ambao wakiwa wanaenda kutafuta maisha nje ya nchi wanat...

KICHAPO MBELE YA MASHUJAA CHAWAPA TAHADHARI SIMBA LEO KUIVAA AFRICAN LYON
YANGA KUSHUSHA MUZIKI KAMILI MBELE YA KENGOLD YA MBEYA KESHO
MUONEKANO WA UKURASA WA NYUMA GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA

SASA imekuwa kawaida, tumerudi kulekule kwa mwanzo. Ninawazungumzia wachezaji wetu ambao wakiwa wanaenda kutafuta maisha nje ya nchi wanatuachia matumaini tele kuwa wanaenda kuitangaza nchi kuwa kwetu kuna vipaji lakini haizidi mwaka kama siyo miezi sita utashangaa wanarudi.


Ni wachache ambao wanavumilia mengi na kupambana lakini wachache wanashindwa na kuamua kurejea nyumbani. Wapo ambao soka linawashinda na wengine kutokana na sababu zao binafsi.


Mbwana Samatta ambaye kwa sasa anakipiga Fenebarche ya Uturuki ni mfano bora na role model kwa wachezaji wengi wazawa kwa sasa na ukiangalia amevumilia mengi hadi amefika hapo alipo.

Aliwahamasisha wengi sana baada ya kutua Genk ya Ubelgiji kisha Aston Villa ya England. Vijana wengi walipambana na kupata nafasi nyingi za kwenda kufanya majaribio na wengine kuanzia vikosi vya vijana.

Lakini hilo rundo pia ni kama linapukutika na kuanza kurejea nyumbani mmoja mmoja, hivi ni kwamba vijana wetu hawawezi kuvumilia au ni nini.


Mchezaji wa zamani wa Yanga, Maka Edward mwaka 2019 alijiunga na timu ya Morocco ya Moghreb Athletic de Tetouan ambapo alisaini mkataba wa miaka minne ambapo aliitumikia kwa miaka miwili na sasa amerudi anapambana kwenye ndondo huko.


Championi lilipomuuliza kama yuko mapumziko na atarudi kwenye klabu yake akasema harudi kwa kuwa ameshindwa maisha ya huko. Alisema hana tena hamu ya kwenda nje kucheza kwa sasa kwani anaona anapoteza muda wake.


Lakini hapo aligusia pia visa kuwa jamaa walisema watamtumia visa baada ya ile ya awali kuisha lakini hawakufanya hivyo, hapohapo anasema kati ya vitu vilivyomkwamisha ni lugha ndio ilikuwa tatizo kubwa sambamba na ugumu wa ligi ambayo alikuwa akicheza ile ya U21 na kikosi cha wakubwa aliishia kukaa benchi.


Hapohapo Nickson Kibabage aliyekuwa Difaâ El Jadida ya Morocco baadaye Berrechid na sasa inadaiwa amerejea nchini baada ya kuachana na timu yake.


Wako wengi ambao wanarudi kimyakimya baada ya kushindwa kama sio kuvumilia basi kushindwa kabisa maisha ya huko nje. Leo hii klabu kubwa zinakuja Tanzania kusajili wachezaji wa kimataifa na sio wazawa.


Mastaa kama Clatous Chama aliyekuwa Simba, Tuisila Kisinda wanasajiliwa kwa fedha nyingi na RS Berkane ya Morocco huku Luis Miquissone naye akitua Al Ahly ya Misri.


Hivi wachezaji wetu hawaoni wivu. Mtu anasajiliwa kutoka nje ya nchi anakuja hapa unacheza naye halafu anasajiliwa tena nje ya nchi kwa fedha nyingi, ninyi hamuoni wivu au ni kuridhika kucheza Simba na Yanga?

Wachezaji wengi tu wamerudi nchini kama  Habibu Kyombo, Yahya Zayd, Farid Musa, Eliud Ambokile, Ramadhan Singano hawa ni kati ya wengi waliowahi kwenda nje na  wakarudi kwa vipindi tofautitofauti.


Labda tuwatafute na hao wengine watuambie kule nje kuna nini, mbona hawadumu kama kaka yao Samatta na Simon Msuva? 



Credit: SALEH JEMBE

Please subscribe to get all sports news instantly
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: WENGI WANARUDI BONGO WAKITOKA NJE, TATIZO NINI CHIPS AMA KUNA LINGINE?
WENGI WANARUDI BONGO WAKITOKA NJE, TATIZO NINI CHIPS AMA KUNA LINGINE?
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEijkkuGfMz6WnShoCSFs4-5gYEzb8_le0TOqyWoTejjjY5jBawD8_AtRNEPdrO8qnZPJLKnhC0O3NQArDkSptvuJkFWApenMIhxTpu5Qa1HYbg2waPNwAJ9krUC0wrHt5egG8fYzZDkWZ7o/w640-h640/Farid+Mussaa.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEijkkuGfMz6WnShoCSFs4-5gYEzb8_le0TOqyWoTejjjY5jBawD8_AtRNEPdrO8qnZPJLKnhC0O3NQArDkSptvuJkFWApenMIhxTpu5Qa1HYbg2waPNwAJ9krUC0wrHt5egG8fYzZDkWZ7o/s72-w640-c-h640/Farid+Mussaa.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/08/wengi-wanarudi-bongo-wakitoka-nje.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/08/wengi-wanarudi-bongo-wakitoka-nje.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy