LIONEL MESSI KUIBUKIA MANCHESTER CITY
HomeMichezo

LIONEL MESSI KUIBUKIA MANCHESTER CITY

BAADA ya taarifa rasmi  ku tolewa na Klabu ya Barcelona Agosti 4 zikieleza kuwa, nyota wao Lionel Messi raia wa Argentina anaondoka klabun...


BAADA ya taarifa rasmi  kutolewa na Klabu ya Barcelona Agosti 4 zikieleza kuwa, nyota wao Lionel Messi raia wa Argentina anaondoka klabuni hapo baada ya kushindikana kusaini mkataba mpya kutokana na sheria ya matumizi ya fedha ya La Liga anatajwa kuingia kwenye anga za Manchester City.

Mtandao wa Barca umesema kuwa Klabu pamoja na Messi (34) mwenyewe wamefikia makubaliano hayo ya pamoja huku wakimshukuru kwa mchango wake mkubwa kwa klabu hiyo tangu ajiunge nayo akiwa mdogo na kumtakia maisha mema huko atakakokwenda.

Messi ambaye anashikilia taji la Ballon d'Or mara sita, alikuwa amekubali kuongeza kandarasi ya miaka mitano Barca huku akikubali pia mshahara wake kupunguzwa kwa asilimia 50 baada ya mkataba wake wa awali kumalizika June 30, mwaka huu.

Messi ametumia asilimia kubwa ya maisha yake ya soka akiwa Barca kuanzia kwenye academy kabla ya kupandishwa timu ya wakubawa mwaka 2003, amecheza michezo 672 na kufunga mabao 778.

Barcelona wamekuwa wakipitia maisha magumu ya kiuchumi kutokana na janga la Corona hali inayowalazimu kwa sasa kupunguza bajeti yao ya msimu ujao kuendana na sheria ya La Liga, pia wanapambana kuwapunguzia wachezaji wao mishahara ambao ni nahodha msaidizi Gerard Pique, Sergio Busquets na Sergi Roberto ambao wapo kwenye mazungumzo ya kupunguziwa asilimia 40 katika mikataba yao ijayo.

Pia wamejaribu kuwauza wachezaji wao kama Antoine Griezmann, Ousmane Dembele, Philippe Coutinho, Samuel Umtiti na Martin Braithwaite lakini hata wakifanya hivyo hali ni mbaya. Hivyo kwa sasa ni vita ya mabosi katika kuisaka saini ya nyota huyo.


Credit: SALEH JEMBE

Please subscribe to get all sports news instantly
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: LIONEL MESSI KUIBUKIA MANCHESTER CITY
LIONEL MESSI KUIBUKIA MANCHESTER CITY
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEghQuHQt77qAwWZGXJY6psO380X1ZebNRYGHZJ_WwHAFXfaQKE9_jYJJee7N2JR13N2rN_BU4mf1pULuNLyp9cRXz4HjtiQPjMHpsCg4sMQEJD7Twtz0fW_R2MlybN15hoiQT615oQ1yQ68/w640-h360/Messi.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEghQuHQt77qAwWZGXJY6psO380X1ZebNRYGHZJ_WwHAFXfaQKE9_jYJJee7N2JR13N2rN_BU4mf1pULuNLyp9cRXz4HjtiQPjMHpsCg4sMQEJD7Twtz0fW_R2MlybN15hoiQT615oQ1yQ68/s72-w640-c-h360/Messi.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/08/lionel-messi-kuibukia-manchester-city.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/08/lionel-messi-kuibukia-manchester-city.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy