MIKEL Arteta, Kocha Mkuu wa Arsenal amesema kuwa walistahili ushindi katika mchezo wa jana ila walishindwa kutumia vema nafasi ambazo wali...
MIKEL Arteta, Kocha Mkuu wa Arsenal amesema kuwa walistahili ushindi katika mchezo wa jana ila walishindwa kutumia vema nafasi ambazo walizipata.
Arsenal ikiwa Uwanja wa Emirates ilikubali kunyooshwa kwa mabao 2-0 jambo lililowafanya wayeyushe mazima pointi tatu.
Unakuwa no mchezo wa pili kwa Arsenal kupoteza kwa kuwa ule wa ufunguzi walipoteza mbele ya Brentford wakiwa ugenini.
Arteta amesema:"Ilikuwa ni lazima tushinde ila namna hali ilivyokuwa mambo yalibadilika. Kipindi cha kwanza tulikuwa na nafasi ya kushinda ila haikuwa hivyo.
"Walipopata bao wapinzani wetu walizidi kulazimisha kupata ushindi na waliweza kufanya kwa nguvu dakika zote 90 hivyo hamna namna ni mbaya kwetu na ukikumbuka kwamba tuliwakosa wachezaji wetu 8 ama 9 hivi,".
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS