Ahukumiwa kifungo cha maisha baada ya kumbaka mtoto wa mwaka mmoja na miezi saba
HomeHabari

Ahukumiwa kifungo cha maisha baada ya kumbaka mtoto wa mwaka mmoja na miezi saba

 Na Amiri Kilagalila,Njombe  Mahakama ya wilaya ya Njombe imemuhukumu kifungo cha maisha jela Steward Mkongwa (33) kwa kosa la kumbaka mto...

Waziri Makamba Aanza Kutekeleza Agizo La Makamu Wa Rais Mkoani Kigoma
Serikali kufuta leseni za uchimbaji madini zisizofanya kazi
Mwandishi wa riwaya Zanzibar Abdulrazak Gurnah ashinda Tuzo ya Nobel katika Fasihi 2021

 Na Amiri Kilagalila,Njombe
 Mahakama ya wilaya ya Njombe imemuhukumu kifungo cha maisha jela Steward Mkongwa (33) kwa kosa la kumbaka mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi saba.

 Katika shauri namba 42 la mwaka  2021 mshtakiwa anadaiwa kufanya kosa la ubakaji kinyume na kifungu cha sheria namba 130 kifungu kidogo cha kwanza na cha pili lakini pia kifungu 131 kifungu kidogo (1)(3) vya kanuni ya adhabu sura namba 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2019.


 Inadaiwa kuwa mnamo tarehe  26 mwezi Julai mwaka 2020 katika mtaa wa Mwembetogwa halmashauri ya wilaya ya Makambako wilayani Njombe mshtakiwa alimbaka mtoto mwenye umri huo.

 Shauri hilo lililosimamiwa na wakili wa serikali Matiko Nyangero lilikuwa na mashahidi wanne upande wa mashtaka na shahidi mmoja upande wa utetezi ambaye ni mshtakiwa katika kesi iliyoendeshwa na hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya Njombe Isaack Mlowe.

 Haimu Mlowe alisema mshtakiwa alikiri kufanya kitendo hicho cha kumuingilia mtoto huyo baada ya mama yake kwenda kuchota maji.

 "Alifanya hivyo kwasababu yeye alikuwa mpangaji pamoja na mama wa huyo pia alikuwa na mazoea na huyo mtoto" alisema Mlowe.

 Kabla ya hukumu hiyo mshtakiwa alipopew nafasi ya kujitetea alisema yeye ana familia inamtegemea kwani ana watoto wawili wa kuwazaa na watoto sita aliyeachiwa na marehemu kaka yake.

 Alisema mke wake aliachana nae kutokana na mitafaruku mbalimbali hivyo mpaka sasa hafahamu watoto hao wanakula ama la.

 "Mimi mwenyewe miguu yangu yote miwili ni mibovu kutokana na kuwa nilipata ajali" alisema Steward.

 Baada ya utetezi huo hakimu Mlowe alimuhukumu mshtakiwa huyo kifungo cha maisha kutokana na kifungu cha sheria namba 131(3) kinachosema mtu yeyote anapotiwa hatiani kwa kosa la ubakaji kwa mtu mwenye umri wa miaka chini ya kumi adhabu yake ni kifungo cha maisha.



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Ahukumiwa kifungo cha maisha baada ya kumbaka mtoto wa mwaka mmoja na miezi saba
Ahukumiwa kifungo cha maisha baada ya kumbaka mtoto wa mwaka mmoja na miezi saba
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhT5R_XgSUmxq7xKWtwwIW3WY2R1nBr_gfjfqPLPwmALOVc0XboJYAFx4-6r8kBSbHuI1wnH6cpyRaAUPo38tOZYn_Alw3h70Xp9ATgjiPYBahtmtiNrQri03RLL0JpfTv4GezZuhyphenhyphenp8XL8/s0/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhT5R_XgSUmxq7xKWtwwIW3WY2R1nBr_gfjfqPLPwmALOVc0XboJYAFx4-6r8kBSbHuI1wnH6cpyRaAUPo38tOZYn_Alw3h70Xp9ATgjiPYBahtmtiNrQri03RLL0JpfTv4GezZuhyphenhyphenp8XL8/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/08/ahukumiwa-kifungo-cha-maisha-baada-ya.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/08/ahukumiwa-kifungo-cha-maisha-baada-ya.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy