Serikali Kuanzisha Kiwanda Cha Chanjo Ya Corona
HomeHabari

Serikali Kuanzisha Kiwanda Cha Chanjo Ya Corona

Na Mwandishi wetu Dodoma Serikali imeanza mchakato wa kutengeneza chanjo ya Virusi vya Corona  hapa nchini ili kupunguza gharama ya kuag...

AUDIO: Ommy Dimpoz & Mwana FA – Baba Akupokee
AUDIO : Alikiba – WOSIA WA MAGUFULI
AUDIO : Tanzania All Stars – Lala Salama (Magufuli)


Na Mwandishi wetu Dodoma
Serikali imeanza mchakato wa kutengeneza chanjo ya Virusi vya Corona  hapa nchini ili kupunguza gharama ya kuagiza nje ya nchi  na kuzifanya ziwe karibu na wananchi.

Akizungumza jana na waandishi wa Habari jijini Dodoma Katibu Mkuu, Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Afya Prof. Abel Makubi amesema kiwanda hicho hakitatengeneza chanjo ya UVIKO tu bali na magonjwa mengine.

"Wataalamu tunao wengi na kiwanda hicho hakitatengeneza chanjo ya UVIKO 19 pekee, hata ikiisha tutaendelea kuzalisha chanjo nchini" alisema Prof. Makubi.

Aidha, Prof. Makubi amesema Serikali haina mpango wa kuwauzia wananchi chanjo ya ugonjwa UVIKO 19 wala kuruhusu mtu yeyote kuingiza chanjo hiyo kinyume na utaratibu utakaowekwa.

Wakati huo huo, Prof. Makubi aliyeambatana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amewataka  viongozi na wasimamizi wa shule kuzingatia mwongozo wa kudhibiti ugonjwa wa UVIKO 19 ili kujikinga bila kuathiri shughuli za kijamii na kiuchumi.

Amesema wakati shule na baadhi ya taasisi za vyuo zinatarajiwa kufunguliwa hapo kesho, mwongozo utakaotumika ni ule ule uliotumika mwaka jana na umepitiwa upya ili kuendana na mahitaji ya sasa

Prof. Makubi  amesema Serikali inalazimika kuwakumbusha viongozi wa shule na Taasisi za Elimu kuimarisha mifumo ya malezi kwenye mabweni, kufanya ukaguzi na ufuatiliaji wa mara kwa mara kuhusu afya za wanafunzi.

"Mambo muhimu ni viongozi wa shule na vyuo kuandaa miundombinu ya maji na upatikanaji wa barakoa kama ilivyokuwa mwaka jana na kuchukua hatua stahiki iwapo kutagundulika kuna maambukizi bila hofu wala taharuki" alisisitiza Prof. Makubi.

Aidha, Prof. Makubi amesisitiza elimu ya kujikinga na ugonjwa huo iendelee kutolewa kwenye maeneo mbalimbali hasa nyumba za ibada, shuleni na vyuoni.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Elimu Prof. Carolyne amesema Wizara kwa kushirikiana na Tamisemi itasimamia miongozo hiyo iliyotolewa na Wizara ya Afya.

"Miundombinu yote ifufuliwe ikiwemo matumizi ya vitakasa mikono, barakoa asilia na maji yanayotiririka" amesisitiza Prof. Carolyne.

MWISHO


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Serikali Kuanzisha Kiwanda Cha Chanjo Ya Corona
Serikali Kuanzisha Kiwanda Cha Chanjo Ya Corona
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgUFNtjStDDSjQJs_hS0rEqYrukZ3zkh2RQRqA009_SJnmy6e2AE6_t2tH8Zn4AvsC0m-LgQ3YXi6lQkbsqYotbDuS-O9iMkh16gFr-vyJ9JuuKkaeBVYbjsn_C_A8sMOqryrFL4N5DOh-3/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgUFNtjStDDSjQJs_hS0rEqYrukZ3zkh2RQRqA009_SJnmy6e2AE6_t2tH8Zn4AvsC0m-LgQ3YXi6lQkbsqYotbDuS-O9iMkh16gFr-vyJ9JuuKkaeBVYbjsn_C_A8sMOqryrFL4N5DOh-3/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/07/serikali-kuanzisha-kiwanda-cha-chanjo.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/07/serikali-kuanzisha-kiwanda-cha-chanjo.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy