SIMBA WAZIDI KUIVUTIA KASI KAIZER CHIEFS, MUGALU AKIMBIZA KWA MABAO
HomeMichezo

SIMBA WAZIDI KUIVUTIA KASI KAIZER CHIEFS, MUGALU AKIMBIZA KWA MABAO

  K ATIKA kuhakisha  Simba inafanikiwa  kupata ushindi dhidi  ya Kaizer Chiefs katika  mchezo wa marudiano wa Robo  Fainali ya Ligi ya Mab...

VIDEO: SHABIKI WA YANGA KUIBUKIA KIGOMA KWA BAISKELI, RATIBA YAKE HII HAPA
VIDEO: NIYONZIMA KUSEPA YANGA, SIMBA KULIPA KISASI KWA YANGA
YANGA: TUTAIPIGA SIMBA PALEPALE KWENYE MSHONO

 KATIKA kuhakisha Simba inafanikiwa kupata ushindi dhidi ya Kaizer Chiefs katika mchezo wa marudiano wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes ametumia muda wake kufundisha kuhusu kucheza mipira ya juu ambayo imeonekana kuwa tatizo katika mchezo wa kwanza uliofanyika nchini Afrika Kusini.

 

Simba katika mchezo wa awali wakiwa ugenini walipoteza kwa kufungwa mabao 4-0 ambapo mchezo wa marudiano unatarajiwa kufanyika kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

 

Katika mazoezi ya mwisho kufanywa na Simba mbele ya mashabiki kwenye Uwanja wa Mo Simba uliopo Bunju, Dar es Salaam, Kocha Gomes aliwatenga mabeki wa pembeni wa timu hiyo na washambuliaji kisha kuwafanyisha mazoezi ya kupiga krosi na washambuliaji kufunga jambo ambalo ni taswira ya kile ambacho wataenda kukifanya dhidi ya Kaizer Chiefs.


Mabeki wa pembeni ambao walikuwa wakipiga krosi walikuwa ni Shomari Kapombe, David Kameta, Mohamed Hussein na Gadiel Michael huku washambuliaji ambao walikuwa wakimalizia krosi hizo ni Chris Mugalu, Meddie Kagere na John Bocco kisha baadaye waliongezeka Clatous Chama na Luis Miquissone.

 

Aidha, katika mazoezi hayo mshambuliaji Mugalu ndiye alikuwa kinara wa kutupia mabao mengi ambapo alifanikiwa kufunga mabao 11 kati ya krosi 17 ambazo alipigiwa katika pande zote mbili za kushoto na kulia.

 

Washambuliaji Meddie Kagere na John Bocco wote walifanikiwa kufunga idadi sawa ya mabao wakifunga 10, ambapo Bocco alifunga mabao hayo katika krosi 16 alizopigiwa huku Kagere yeye akifunga idadi hiyo katika krosi 17 alizopigiwa.

 

Kwa upande wa asisti beki wa kushoto, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ ndiye aliyekuwa kinara wa pasi za mabao ambapo alifanikiwa kutoa asisti 10 huku Kapombe akitoa 9, Gadiel alifanikiwa kutoa pasi 7 huku Kameta akifanikiwa kutoa pasi 5 za mabao.


Aidha, Gomes alionekana akiwasisitizia mabeki wa timu hiyo kupiga krosi za aina yote za juu na chini kwa ufasaha ili kuhakikisha kuwa wanapata mabao ya aina yote kuelekea mchezo huo.



Credit: SALEH JEMBE

Please subscribe to get all sports news instantly
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: SIMBA WAZIDI KUIVUTIA KASI KAIZER CHIEFS, MUGALU AKIMBIZA KWA MABAO
SIMBA WAZIDI KUIVUTIA KASI KAIZER CHIEFS, MUGALU AKIMBIZA KWA MABAO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgktBMmbmGtACvqFxV_zjgs_2Ng7BxNHPx0R1nj6lXVaelcq2XFBA3ZIMbyh__Tn8sQTu4G_sLBJAvpGtmTgpMk66O_Wqn9YZpcFI415aeA3Ytt1KY1X4sDq-iUUn_KgfN7rB_LvkOCbfeP/w640-h428/Manula+mazoezi.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgktBMmbmGtACvqFxV_zjgs_2Ng7BxNHPx0R1nj6lXVaelcq2XFBA3ZIMbyh__Tn8sQTu4G_sLBJAvpGtmTgpMk66O_Wqn9YZpcFI415aeA3Ytt1KY1X4sDq-iUUn_KgfN7rB_LvkOCbfeP/s72-w640-c-h428/Manula+mazoezi.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/05/simba-wazidi-kuivutia-kasi-kaizer.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/05/simba-wazidi-kuivutia-kasi-kaizer.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy