LEO Jumanne, Julai 13, 2021 Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) itakabidhi Kombe la Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) kwa msimu wa 2020-2021 katik...
LEO Jumanne, Julai 13, 2021 Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) itakabidhi Kombe la Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) kwa msimu wa 2020-2021 katika Uwanja wa Uhuru.
Simba Queens ni mabingwa wa taji hilo ambapo wanatarajiwa kukabidhiwa leo taji lao rasmi.
Ofisa Habari wa Simba Queens, Monalisa amesema kuwa mashabiki wajitokeze kwa wingi, Uwanja wa Uhuru kushuhudia timu hiyo ikikabidhiwa taji hilo ambalo ni la pili kwao.
Zoezi la Kukabidhiwa Kombe litatanguliwa na mchezo wa kirafiki kati ya Timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) na Simba Queens utakaoanza saa 9:30 mchana.
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS