Kuanzishwa Kwa Kiwanda Cha Kusafisha Madini Cha GGR Kuchangamsha Uchumi Wa Geita-Waziri Biteko
HomeHabari

Kuanzishwa Kwa Kiwanda Cha Kusafisha Madini Cha GGR Kuchangamsha Uchumi Wa Geita-Waziri Biteko

  Imeelezwa kuwa kuanzishwa kwa kiwanda cha Kusafisha Madini cha Mkoani Geita kitaongeza na kuchangamsha uchumi wa mkoa na Taifa kwa uju...

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Novemba 23
Majaliwa: Fedha Za Miradi Zitumike Kama Ilivyokusudiwa
Rais Samia atunuku Nishani na Shahada kwa Wahitimu wapya JWTZ Monduli Arusha

 


Imeelezwa kuwa kuanzishwa kwa kiwanda cha Kusafisha Madini cha Mkoani Geita kitaongeza na kuchangamsha uchumi wa mkoa na Taifa kwa ujumla wake.

Waziri wa Madini Mhe Doto Biteko ameeleza hayo  jana tarehe 8 Mei 2021 wakati akiweka Jiwe la Msingi katika kiwanda cha kusafisha madini cha GGR akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Geita.

Waziri Biteko amesema kuwa kiwanda hicho cha kisasa na cha kwanza cha aina yake barani Afrika kimekusudia kuimarisha nyanja za kusafisha dhababu nchini jambo litakaloimarisha soko la uhakika la uuzaji wa madini na kuiwezesha Benki kuu kununua madini yenyewe.

Amesema kuwa ni fahari kubwa katika sekta ya madini kwani uwekezaji huo ni mkubwa na muhimu utakaokijibu ndoto za serikali katika kuwakomboa wachimbaji wadogo wa madini.

Mhe Biteko amewaasa wachimbaji kuwa na ushirikiano na kupendana kwani uchumi wa nchi hauwezi kuimarika kwa baadhi ya wachimabji kuwachukia waliofanikiwa.

“Nasikitika kuna vijiwe vimegawanyika kazi yao kusuka majuku na kuwachukia wengine waliofanikiwa, Ushindeni ubaya kwa wema, aliyefanikiwa tumuombee Mungu amsogeze mbele” Amekaririwa Waziri Biteko

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Gabriel Robert amesema kuwa dhahabu inayouzwa katika mkoa huo imeamsha ari kwa wawekezaji kuanza kuwekeza katika sekta mbalimbali jambo linaloimarisha uchumi wa mkoa.

Amesema kuwa mkoa wa Geita pamoja na mambo mengine lakini ni sehemu sahihi kwa ajili ya kuwekeza katika sekta ya madini.

Awali akisoma taarifa ya kiwanda cha kusafisha madini cha GGR Kaimu Mkurugenzi wa Bodi Mhandisi Athuman Mfutakamba amesema kuwa kiwanda hicho kilipewa leseni ya kusafisha dhahabu No RFL 001/2019 iliyotolewa na Wizara ya Madini tarehe 16 Julai 2019 na kina uwezo wa kusafisha 400 kg kwa siku na kufikia tani 200 kwa mwaka kwa kiwango cha juu kabisa na kukidhi kufikia kiwango cha usafi wa asilimia 999.9 na 999.5

Amesema kampuni imejiimarisha ipasavyo kutekeleza wajibu huo kwa kufunga vifaa/mashine za kusafisha dhahabu vya kisasa na vyenye viwango vya hali ya juu vinavyokidhi viwango vya kimataifa.


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Kuanzishwa Kwa Kiwanda Cha Kusafisha Madini Cha GGR Kuchangamsha Uchumi Wa Geita-Waziri Biteko
Kuanzishwa Kwa Kiwanda Cha Kusafisha Madini Cha GGR Kuchangamsha Uchumi Wa Geita-Waziri Biteko
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiV-hs0OBayJ8vZwylmSQ1xnlTSIiOX4RjyUyBIJ28KdY2_A3_L2f1AjcoKuQnqEPSHFOZ-0-TXaqHMfGUfRpNRrKc8oJnEsRtgOf1b4BwWECLdryCvZ-wEeWULlU27jscq38JIEzAv1FFy/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiV-hs0OBayJ8vZwylmSQ1xnlTSIiOX4RjyUyBIJ28KdY2_A3_L2f1AjcoKuQnqEPSHFOZ-0-TXaqHMfGUfRpNRrKc8oJnEsRtgOf1b4BwWECLdryCvZ-wEeWULlU27jscq38JIEzAv1FFy/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/05/kuanzishwa-kwa-kiwanda-cha-kusafisha.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/05/kuanzishwa-kwa-kiwanda-cha-kusafisha.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy