AKILI ZA GOMES WA SIMBA ZIPO KWA WATANI ZAKE WA JADI YANGA
HomeMichezo

AKILI ZA GOMES WA SIMBA ZIPO KWA WATANI ZAKE WA JADI YANGA

LICHA ya kwamba amekiongoza kikosi chake kutinga hatua ya robo fainali baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya AS Vita,  Didier  Gomes hesa...

MSUVA AJIPA MATUMAINI KIBAO CAF
KOCHA MANCHESTER UNITED ABWAGA MANYANGA
AUSSEMS: UBORA UTAIBEBA SIMBA SC KWA KAIZER

LICHA ya kwamba amekiongoza kikosi chake kutinga hatua ya robo fainali baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya AS Vita, Didier Gomes hesabu zake zipo ndani ya Ligi Kuu Bara kuhakikisha anaishusha Yanga kileleni.

 

Gomes ambaye msimu huu ana kibarua cha kutetea taji la Ligi Kuu Bara, Mei 8, mwaka huu atakutana na Yanga kwa mara ya kwanza tangu awe kocha wa Simba.

 

Kabla ya timu hizo kukutana, Simba itacheza mechi tano za ligi ambazo ni sawa na dakika 450, huku Yanga iliyo chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Juma Mwambusi, ikiwa na dakika 360, sawa na mechi nne


Mechi za Gomes ni dhidi ya Mtibwa Sugar (Aprili 14), Mwadui FC (Aprili 18), Kagera Sugar (Aprili 21), Gwambina (Aprili 24) na Dodoma Jiji (Aprili 27), kisha ndiyo anakutana na Yanga.

 

Kwa upande wa Mwambusi, yeye atakuwa na kazi mbele ya KMC (Aprili 10), Biashara United (Aprili 17), Gwambina (Aprili 20), Azam (Aprili 25), kisha atapambana na Simba ya Gomes.

 

Gomes raia wa Ufaransa, ameliambia Spoti Xtra kuwa: â€œMechi zote kwetu ni muhimu kupata pointi tatu, kwani ukitazama tunahitaji kuongoza ligi ili kufikia lengo la kutwaa kombe, haitakuwa kazi rahisi, nimewaambia wachezaji wana kazi kubwa ya kufanya," .

 

Msimamo wa Ligi Kuu Bara kwa sasa unaonesha Yanga inaongoza ikiwa na pointi 50 baada ya kucheza mechi 23, huku Simba ikiwa ya pili ikikusanya pointi 46 ikishuka dimbani mara 20.



Credit: SALEH JEMBE

Please subscribe to get all sports news instantly
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: AKILI ZA GOMES WA SIMBA ZIPO KWA WATANI ZAKE WA JADI YANGA
AKILI ZA GOMES WA SIMBA ZIPO KWA WATANI ZAKE WA JADI YANGA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhK830ybJ4rk0FLCbi3ymFeuSH96_sCSW75A9nC01PJDqnwabEZmyC0aN5SAG4Yi6J3gdTKcauFPlnHJx6b4Ab5D9s6qCa3ehO20moQsQlrbH-cfi34WXd4FtOZygSiWWxkywu6j5TumLNC/w640-h606/Gomez+kazini.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhK830ybJ4rk0FLCbi3ymFeuSH96_sCSW75A9nC01PJDqnwabEZmyC0aN5SAG4Yi6J3gdTKcauFPlnHJx6b4Ab5D9s6qCa3ehO20moQsQlrbH-cfi34WXd4FtOZygSiWWxkywu6j5TumLNC/s72-w640-c-h606/Gomez+kazini.JPG
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/04/akili-za-gomes-wa-simba-zipo-kwa-watani.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/04/akili-za-gomes-wa-simba-zipo-kwa-watani.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy