Baraza la Seneti lapiga kura kuendelea na kesi ya Trump
HomeHabari

Baraza la Seneti lapiga kura kuendelea na kesi ya Trump

Baraza la Seneti nchini Marekani limepiga kura kuendelea na mchakato wa mashitaka dhidi ya rais wa zamani Donald Trump, likisema mchakato ...

Habari Zilizopo Katika mgazeti ya Leo july 25
Serikali Yatoa Maelekezo Hatua Ya Kudhibiti Ajali Barabarani
Waziri Mkuu Akagua Maandalizi Ya Siku Ya Mashujaa Dodoma

Baraza la Seneti nchini Marekani limepiga kura kuendelea na mchakato wa mashitaka dhidi ya rais wa zamani Donald Trump, likisema mchakato huo ni wa kikatiba.

Baraza la Seneti lilipiga kura 56 kwa 44 za kuendelea na kesi dhidi ya Trump, likizipinga hoja za mawakili wake kwamba rais hawezi kushitakiwa pindi anapomaliza muda wake.

Maseneta ambao waliapishwa kama wazee wa baraza, walipitia picha za vidio za wafuasi wa Trump wakipambana na polisi, kuvamia kumbi za bunge na kupeperusha bendera za Trump. Pia kuliwasilishwa vidio za Trump mwenyewe akiwahimiza wafuasi wake kabla ya uvamizi kuwa wapambane hadi tone la mwisho kupinga kushindwa kwake kwenye uchaguzi wa Novemba 3.

Kiongozi mkuu wa mashitaka hayo Jammie Raskin aliwaeleza maseneta kwamba kesi hiyo itawasilisha "ukweli mgumu" dhidi ya Trump. "Rais Trump ametuma mawakili wake hapa leo kujaribu kuzuia Bunge la Seneti kusikia ukweli wa kesi hii. Wanataka kuzima kesi kabla hata ya ushahidi wowote kutolewa. Hoja yao ni kwamba ikiwa unafanya makosa ya kushitakiwa katika wiki zako za mwisho mamlakani, basi unafanya ukiwa na kinga ya kikatiba na unanusurika".

Mawakili wa Trump wameendelea kuushambulia mchakato huo wakisema ni kinyume na katiba na kwamba ni juhudi za kumzuia kiongozi huyo kuwania tena nafasi ya urais.

 Wakili anayeongoza jopo la utetezi upande wa Trump Bruce Castor, amesema mashitaka dhidi ya rais huyo hayahitajiki tena kutokana na kwamba kiongozi huyo aliondolewa madarakani kupitia kura na hivyo lengo la kikatiba tayari limefanikiwa.

Trump anakabiliwa na shtaka moja la uchochezi wa uasi baada ya wafuasi wake kuvamia majengo ya bunge mnamo mwezi Januari. Alishitakiwa na baraza la wawakilishi Januari 13.

Maseneta wengi wa Republican wameashiria kuwa hawatopiga kura ya kumtia hatiani Trump na hivyo kuna uwezekano akavuka kiunzi hicho. 

Ili aweze kukutwa na hatia kunahitajika theluthi mbili ya wingi wa kura kwa maana kwamba angalau maseneta 17 wa Republican itabidi wajiunge na wenzao 48 wa Democatrs katika kupiga kura dhidi ya Trump ambaye amesalia kuwa mtu aliye na nguvu ndani ya chama chake licha ya kuondoka mamlakani.

Credit:DW



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Baraza la Seneti lapiga kura kuendelea na kesi ya Trump
Baraza la Seneti lapiga kura kuendelea na kesi ya Trump
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhZv81kIETQZT3sr3G3nQKHBIjj8tl81mXBNSPcAMH7MKmJyMU4TvOOlm8rWz2rKiS-azaLRBPMBd710Pn-opAYr6A5sTk94Q8uor_k216NfSKY1FhbVKFYwj5qq0lM9l7HouCdD_GkHQ1G/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhZv81kIETQZT3sr3G3nQKHBIjj8tl81mXBNSPcAMH7MKmJyMU4TvOOlm8rWz2rKiS-azaLRBPMBd710Pn-opAYr6A5sTk94Q8uor_k216NfSKY1FhbVKFYwj5qq0lM9l7HouCdD_GkHQ1G/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/02/baraza-la-seneti-lapiga-kura-kuendelea.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/02/baraza-la-seneti-lapiga-kura-kuendelea.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy