Wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya Kimataifa ambao pia ni Mabingwa wapya wa ligi kuu ya Tanzania bara Dar es salaam...
Wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya Kimataifa ambao
pia ni Mabingwa wapya wa ligi kuu ya Tanzania bara Dar es salaam Young
Afrika Usiku huu wamekubali kuondolewa katika michuano ya Kombe la
Shirikisho barani Afrika baada ya kufungwa bao moja bila katika mtanange
wa maruduiano dhidi ya Etoile Du Sahel.
Yanga ambao walikuwa ugenini hawakuweza kuonyesha hari ya ugeni kwani walikuwa wakishambulia mwanzo mwisho lakini bahati ikadondokea kwa Waarabu hao ambao hadi mwisho wa mchezo walikuwa pungufu baada ya mchezaji wao kupewa kadi Nyekundu kufatia kuwa na kadi mbili za njano.
Katika mtanange huo ambao Yanga wanashambulia kwa kasi bila kujali kuwa wapo ugenini kunako dakika ya 9 wanapata free kick ambayo anapiga Ngassa lakini inakosa macho na kutoka nje.
Yanga ambao walikuwa ugenini hawakuweza kuonyesha hari ya ugeni kwani walikuwa wakishambulia mwanzo mwisho lakini bahati ikadondokea kwa Waarabu hao ambao hadi mwisho wa mchezo walikuwa pungufu baada ya mchezaji wao kupewa kadi Nyekundu kufatia kuwa na kadi mbili za njano.
Katika mtanange huo ambao Yanga wanashambulia kwa kasi bila kujali kuwa wapo ugenini kunako dakika ya 9 wanapata free kick ambayo anapiga Ngassa lakini inakosa macho na kutoka nje.
Dakika ya 18 Etoile Du sahel walikosa bao baada ya mchezaji wake kuwaadaa mabeki na kupiga mpira ambao ulitoka nje kidogo ya lango la Yanga.
Dakika ya 22 kipa wa Yanga Deogratius Munish Dida anafanyiwa matibabu baada ya kuumizwa na washambuliaji wa wapinzani wao wakiwania mpira wa juu uliopigwa free kick.
Dakika ya 24 Dida anaokoa bao la wazi baada ya kuutema mpira na kumaliziwa na kuwa kona.
Eto el wanapata bao la kwanza dakika ya 24 baada ya mchezaji wake kumalizia kwa kichwa krosi iliyopigwa na kutoka winga ya kulia.
Dakika ya 33 Sherman anakosa bao baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Ngassa lakini akapaisha juu mpira.
Dakika ya 42 Twite anaokoa bao baada ya kupiga kichwa mpira ambao ulikuwa unaingia langoni.
Hata hivyo katika Yanga katika kipindi cha pili watakuwa na uwezekano wa kuongeza bao endapo wataendelea kushambulia kwa kasi kwani wanafaida ya kuwa wengi baada ya mchezaji wa Etoile Du nSahel kutolewa kwa kadi Nyekundu baada ya kumfanyia madhambi Msuva
Baada ya kipindi cha pili kuanza kwa kasi kubwa Yanga wakitafuta bao la kusawazisha, Kunako dakika ya 48 vijana hao wa Jangwani wanakosa bao la wazi baa ya kipa wa Etoile kujichanganya lakini Sherman akachelewa kumalizia kazi hiyo.
Dakika ya 65 Kocha Hans Van Pluijm anaamua kumpumzisha Khap Sherman na nafasi yake anaingia Hussein Javu.
Amissi Tambwe anakosa bao baada ya kupenyezewa pasi ya chini lakini akapiga mpira unageuka chakula ya Kipa wa Etoile Du Sahel dakika ya 70.
Kelvin Yondani anapewa kadi ya Njano baada ya kumfanyia madhambi mshambuliaji wa waarabu hao ikiwa ni dakika ya 73.
Dakika ya 82 AndreyCoutinho anaingia kuchukua nafasi ya Salum Telela.
Hadi dakika ya ya mwisho mwamuzi
anapuliza kipenga Yanga wanaambulia kipigo cha bao 1-0 kutok akwa
wenyeji wao Etoile Du Sahel na kukubali kuondolewa kwenye michuano ya
kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Kufatia matokeo hayo Yanga
inakuwa imeondolewa kwa jumla ya mabao 2-1 kufatia mchezo wa kwanza
uliopigwa jijini Dar es salaam kumalizika kwa sare ya 1-1.
COMMENTS