Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu. Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii iko hatarini kutopitishwa, baada ya K...
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu.
Bajeti
ya Wizara ya Maliasili na Utalii iko hatarini kutopitishwa, baada ya
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira kukataa kwa
mara pili kuijadili.
Wabunge
wa Kamati hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wake, James Lembeli, walifikia
uamuzi wa kutoijadili tena na kuwaamuru viongozi wa Wizara hiyo
wakiongozwa na Waziri Lazaro Nyalandu (pichani), kurudi tena baada ya
wiki moja wakiwa wametekeleza maagizo yaliyotolewa na kamati.
Maagizo
hayo ni pamoja na kukaidi amri ya Mahakama Kuu ya kukataa kuanza mara
moja utekelezaji wa tozo mpya kwenye Hifadhi za Taifa.
Lingine
ni utaratibu wa kiingilio kwenye hifadhi na kwamba tozo iliyotakiwa ni
kila mtalii anapoingia anapoingia anatozwa kiingilio na akitoka na
kutaka kuingia tena ni lazima alipe.
Agizo
lingine ni mgogoro wa mipaka kwenye Hifadhi ya Taifa ya Saadani. Kamati
iliagiza kuwa mipaka ya hifadhi hiyo ibaki kama ilivyokuwa tangu awali,
lakini kinyume chake, wizara imemega sehemu ya ardhi na kuitafutia hati
miliki.
Kutokana
na maagizo hayo, Kamati hiyo juzi iliwaagiza viongozi hao wa Wizara ya
Maliasili na Utalii kufika katika kamati hiyo jana wakiwa na maelezo
yote.
Licha
ya maagizo hayo, viongozi wa Wizara hiyo walipofika katika Kamati hiyo
jana hawakuwa wametekeleza maagizo hayo, hivyo waliamliwa kurudi Mei 14
mjini Dodoma wakiwa na maelezo kamili.
Akitoa
sababu za kushindwa kuwasilishwa na kutekeleza maagizo hao, Waziri
Nyarandu alieleza kuwa muda wa siku moja waliopewa na Kamati ni mdogo
kutekeleza maagizo yote.
COMMENTS