Mkali wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson amevunja ukimya na kupinga vikali tetesi za ujauzito wake kuhusishwa na mmoja wa mawaziri...
Mkali wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson amevunja ukimya na
kupinga vikali tetesi za ujauzito wake kuhusishwa na mmoja wa mawaziri
wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete akibainisha kuwa jambo hilo linautesa moyo
wake.
Akizungumza na Risasi jijini Dar, Aunt alifunguka
kwamba, mbali na kumzushia juu ya ujauzito huo, kuwa mara ya kwanza watu
asiowajua walieneza uvumi kuwa alikwenda nchini Marekani na mheshimiwa
huyo lakini aliwapuuza kwa kuwa alikwenda kwa kazi yake ya sanaa.
“Kuna binadamu hawajali maumivu ya mtu mwingine, inawezekanaje mtu
aanze kuropoka kitu kizito kama hicho tena mtu na familia yake, sasa mtu
ambaye ndiye muhusika wa ujauzito huu anajisikiaje?
“Ukweli mimba yangu siyo ya waziri, ifahamike kuwa namheshimu sana
mheshimiwa, najisikia vibaya mtu anapoeneza kitu cha namna hiyo,”
alisema Aunt kwa uchungu mkubwa.
Aunt alitiririka kwamba, mbali na uvumi huo, pia alishangazwa na
baadhi ya wabunge waliothubutu kuzungumza kuhusu yeye na waziri huyo
tena bungeni kwenye kujadili vitu vya msingi badala yake wanazungumza
mambo ambayo hayana kichwa wala miguu.
“Hivi inawezekana kweli kabisa wabunge ambao tunawaheshimu wanakwenda kuzungumza vitu vya ajabu bungeni?
“Wamenifanya nisiwe naangalia hata hilo bunge kabisa,” alisema Aunt.
Staa huyo alimalizia kuwa mambo hayo yanampa wakati mgumu na kumuumiza
kwa sababu madai yanayozungumzwa ni mazito huku yakiwa hayana chembe ya
ukweli zaidi ya kuleta mfarakano kwenye familia ya waziri huyo ambaye
pia ni mbunge.
Mbali na waziri huyo, pia Aunt alikanusha kuwa mimba kubwa aliyonayo
si ya yule mcheza shoo wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’, Mose Iyobo
kama wengi wanavyodai.
Kuhusu hilo, Risasi lilizungumza na
Mose Iyobo ambaye alisema kuwa anachojua ujauzito ni wa kwake lakini
akashangazwa na uzushi usiokuwa na kichwa wala miguu.
Baadhi ya mashabiki wa Aunt waliozungumza na Risasi walionesha
kubaki na alama ya ulizo kwamba kama Aunt anamruka Mose Iyobo na
amekasirishwa na tetesi za kuhusishwa na waziri huyo ambaye ni mume wa
mtu huku mumewe, Sunday Demonte akidaiwa kufungwa Dubai, je, mimba hiyo
ni ya nani?
Credit: Risasi/gpl
Credit: Risasi/gpl
COMMENTS