Emmanuel Okwi wa Simba (kulia) akikwatuliwa na beki wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' katika mechi baina ya timu hizo leo kwenye U...

Emmanuel Okwi wa Simba (kulia) akikwatuliwa na beki wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' katika mechi baina ya timu hizo leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Simba ilishinda kwa bao 1-0 lililofungwa na Okwi.

Abdi Banda wa Simba (kulia) akiondoka na mpira huku akikabwa na kiungo Haruna Niyonzima wa Yanga.

Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' akizozana jambo na mwamuzi wa mechi ya Yanga na Simba, Martine Saanya.

Kipa wa Yanga, Ally Mustapha 'Barthez' akiudaka mpira huku akishuhudiwa na kiungo wa Simba, Ramadhani Singano (katikati) na beki wa Yanga, Oscar Joshua.

Beki wa Yanga, Mbuyu Twite akiondoa mpira huku akizongwa na Emmanuel Okwi wa Simba.

Mashabiki wa Yanga wakionekana kusisitiza jambo katika mchezo huo wa leo kati ya timu yao dhidi ya Simba.
Timu ya Simba SC ya jijini Dar es Salaam, leo
imeendeleza ubabe dhidi ya Yanga SC baada ya kuifunga goli 1-0 goli
lililowekwa kimiani na mshambuliaji Emmanuel Okwi katika dakika ya 53
kipindi cha pili
Mechi hiyo ya ligi kuu imefanyika katika uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam ikuhudhuriwa
COMMENTS