Msanii wa filamu bongo Monalisa aanika vyanzo vyake vya pesa Baada ya Lulu kuponda kuwa filamu hazilipi wanawake
HomeMatukio

Msanii wa filamu bongo Monalisa aanika vyanzo vyake vya pesa Baada ya Lulu kuponda kuwa filamu hazilipi wanawake

Kuna baadhi ya mastaa wanaojua kuyatumia majina yao, kwani licha ya kuwa mwigizaji na mtangazaji wa redio, Yvonne Ch...

WALIMU MBEYA WAANDAMANA KUDAI HAKI ZAO
Lulu amtaka Marlaw kurudi kwenye game
Ajuza miaka 90: anasoma darasa la nne. Je Elimu Kweli Haina Mwisho?

Kuna baadhi ya mastaa wanaojua kuyatumia majina yao, kwani licha ya kuwa mwigizaji na mtangazaji wa redio, Yvonne Cherry ‘Monalisa’ hafanyi kazi hizo pekee bali ana kampuni inayobeba tenda mbalimbali katika sekta za umma na binafsi.

Akizungumza na Gazeti la Mwananchi,Monalisa alisema kuwa anapenda kufanya mambo yake chinichini ndiyo maana walio wengi hawajui anayoyafanya katika jamii.

Hata hivyo, alibainisha kuwa anafanya kazi katika kampuni zaidi ya tatu kila siku na anatenga muda wa kuwa na familia yake, hiyo ndiyo sababu pekee inayomwepusha kufanya mambo yasiyofaa.

“Mambo yangu huwa nafanya kimyakimya siyo lazima upige makelele watu wakujue taratibu watu watakujua tu lazima, nina kampuni yangu mwenyewe Sherry Company Limited na sasa hivi ni meneja wa Manday Entertainment. Hii ni kampuni mpya wa filamu na burudani, tuna studio za audio na video tunataka pia kuanza na usambazaji wa filamu,” alisema.

Monalisa alisema kupitia kampuni yake ametengeneza filamu nyingi. “Binti Nusa 1,2,3 nilitengeneza kupitia filamu yangu, mara nyingi nafanya tenda mbalimbali ingawa sijajitangaza sana,” alisema na kuongeza: “Inatengeneza vitu mbalimbali katika sekta za umma na binafsi. Ukiachana na kampuni hizi mbili, nafanya kazi ya utangazaji na pia tamthilia na filamu, niko bize kwa kweli.”

Kuhusu tasnia ya filamu, Monalisa alisema hakuna elimu ambayo haijatolewa kuhusu maisha ya kupendana kwa wanasanii.

“Tumeshahubiri umoja, watu tupendane kwangu mimi naona hapa kila mtu afanye kwa nafasi yake ili tufikie mahala tunapopataka,” alisema Monalisa na kuongeza: “Kuwa wasambazaji ni lazima kuwa makini na masilahi ya msanii mmoja mmoja.

“Wasambazaji nao wanataka kulifanya soko letu liwe gumu, nilikuwa kinyume na wao, namshukuru Mungu wizara ilishatoa tamko kuhusu bei ya filamu iliyopangwa na kampuni ya kusambaza filamu ya Steps kwamba isitishwe.

Filamu hazitauzwa tena Sh1,500, natumaini wataendelea na msimamo wao huohuo na watakuja na bei elekezi ili sote tufahamu kitakachokuwa kikiendelea.
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Msanii wa filamu bongo Monalisa aanika vyanzo vyake vya pesa Baada ya Lulu kuponda kuwa filamu hazilipi wanawake
Msanii wa filamu bongo Monalisa aanika vyanzo vyake vya pesa Baada ya Lulu kuponda kuwa filamu hazilipi wanawake
http://www.bongomovies.com/public/uploads/MONALISA224.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2015/01/msanii-wa-filamu-bongo-monalisa-aanika.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2015/01/msanii-wa-filamu-bongo-monalisa-aanika.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy