‘ Shukrani ’ ni kitu muhimu na ni jambo jema sio hapa dunia tu hata huko mbinguni (Kwa wanoamini), ni vyema k...
‘Shukrani’
ni kitu muhimu na ni jambo jema sio hapa dunia tu hata huko mbinguni
(Kwa wanoamini), ni vyema kumshuru Mungu kwa kila jambo na vile vile
kuwashukuru watu ambao kwa namna moja au nyingine wamekusaidia
kufikia hapo ulipo.
Mrembo
na mwigizaji wa filamu, Irene Uwoya amekuwa sio mchoyo wa fadhira kwa
kumshukuru hadharani muongozaji na mwigizaji wa filamu Vicent Kigosi
‘Ray’ kwa kuwa ni moja ya watu waliomsaidia katika sanaa.
Kupitia
ukurasa wake wa kwenye mtandao wa INSTAGRAM, Irene Uwoya aliweka picha
hiyo hapo juu, akiwa na Ray na kuandika maneno haya.
“Siku zote siwezi kuacha Kuku heshimu wewe ni mtu muhimu sana kwenye safari yangu ya sanaaa!GOD BLESS UUU”
Kitendo
hiki cha Irene kilipongezwa wengi kuwa ni jambo la msingi na lakuigwa
na sio wasanii tu bali watu wote, kwani ni mara chache sana watu kuwa
shukuru hadharani kama hivi watu amabo walisaidia katika mafaniokio
yao.
Hili ni jambo jema safi sana Irene na heshima kwako Ray
COMMENTS