Ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa bwawa la Julius Nyerere wafikia asilimia 99.55
HomeHabariTop Stories

Ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa bwawa la Julius Nyerere wafikia asilimia 99.55

Uongozi wa Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO) Desemba 19, 2024 umetembelea Mradi wa Kufua umeme wa Bwawa la Julius Nyerere kujionea kasi y...

Uongozi wa Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO) Desemba 19, 2024 umetembelea Mradi wa Kufua umeme wa Bwawa la Julius Nyerere kujionea kasi ya maendeleo ya ujenzi unavyoendelea na kuweka mkazo kwa wasimamizi kuhakikisha usimikaji wa mashine nne zilizobakia unafanyika ipasavyo ili umeme utakapozalishwa uingizwe kwenye Gridi ya Taifa kwa mafanikio yatakayoleta tija inayotarajiwa kwa watumiaji wa umeme.

 

Akizungumza wakati wa Ziara hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Mha. Gissima Nyamo-Hanga amesema kwasasa jumla ya mashine tano (05) zimekamilika kwa asilimia 100 yaani mashine namba 9, 8, 7, 6 na 5 na tayari zimeanza uzalishaji wa umeme.

 

” Tumetembelea mradi huu kujionea shughuli zinazoendelea na kuweka msisitizo wa usimamizi bora kwa maeneo ambayo bado hayajakamilika ambapo utekelezaji kwa ujumla umefikia asilimia 99.55 huku shughuli za uzalishaji wa umeme zikiwa zimeanza na wastani wa megawati 1175 zinazozalishwa kutoka mashine tano za mradi huu zimeingizwa kwenye grid ya Taifa ” ameeleza Mha. Gissima.

 

Amebainisha kuwa utekelezaji wa usimikaji wa mashine namba 4 umefikia asilimia 100 ambapo kwasasa mashine hiyo ipo kwenye majaribio huku mashine namba 3 ikiwa kwenye asilimia zaidi ya 87 za usimikwaji, asilimia ambazo zinadhihirisha kuwa kiwango cha utendaji kazi ni kizuri .

 

Amewahimiza wasimamizi wa mradi kuhakikisha wanaendeleza bidii kusimamia maeneo ambayo bado hayajakamilika kuhakikisha kazi inafanyika kwa viwango vilivyoainishwa wakati wa usanifu wa mradi huo.

 

” Niwaombe msimamie vizuri kuhakikisha ufanyaji kazi wa mashine unakuwa ni mzuri ili umeme unaoendelea kuzalishwa unapoungwa kwenye Gridi ya Taifa usilete changamoto yoyote ” amesisitiza Mha. Gissima.

 

Katika hatua nyingine, Mha. Gissima ameishukuru , Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Wizara ya Nishati na viongozi wake wote kwa namna ambavyo mara zote imeunga mkono kwa kutoa fedha na ushirikiano katika kusimamia utekelezaji wa mradi mpaka kufikia hatua iliyopo sasa pamoja na miradi mingine mingi inayoendelea nchini .

 

” Ninawaahidi watanzania wenzangu kuwa, sisi kama viongozi wa TANESCO tutahakikisha tunasimamia mradi huu kwa dhati na umadhubuti mkubwa ili kuhakikisha unakamilika kwa wakati na kuleta tija ya kiuchumi na kijamii katika taifa letu la Tanzania” alihitimisha Mha. Gissima.

 

Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere tayari umeanza kuleta matumaini makubwa ya Kuimarisha hali ya upatikanaji wa umeme nchini ikiwa ni kati ya Juhudi kubwa za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt Samia Suluhu Hassan.

 

The post Ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa bwawa la Julius Nyerere wafikia asilimia 99.55 first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/G2Nbvxw
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa bwawa la Julius Nyerere wafikia asilimia 99.55
Ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa bwawa la Julius Nyerere wafikia asilimia 99.55
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2024/12/IMG-20241220-WA0018-950x634.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2024/12/ujenzi-wa-mradi-wa-kufua-umeme-wa-bwawa.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2024/12/ujenzi-wa-mradi-wa-kufua-umeme-wa-bwawa.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy