CRISTIANO RONALDO AACHANA NA MCHUMBA WAKE, KISA……………
HomeMichezoKimataifa

CRISTIANO RONALDO AACHANA NA MCHUMBA WAKE, KISA……………

Inaaminika Cristiano Ronaldo amethibitisha kuachana na Irina Shayk SIRI imefichuka!. Cristiano Ronaldo alisherehekea mwaka mpya peke ...

Suicide bomber kills 4 people in Somalia's capital
Korea Kazkazini yaionya Marekani
Shahidi wa ICC apatikana ameuawa Kenya
Inaaminika Cristiano Ronaldo amethibitisha kuachana na Irina Shayk
SIRI imefichuka!. Cristiano Ronaldo alisherehekea mwaka mpya peke yake baada ya mchumba wake, Mrusi kutokwenda katika sherehe ya siri aliyoandaa nyumbani kwao Madeira, gazeti maarufu la Ureno la Correio da Manha rimeripoti.
 
Gazeti hilo limetoa habari jana na kuthibitisha kuwa familia ya Ronaldo imevunjika baada kukosekana kwa maelewano baina ya Ronaldo na mpenzi wake Irina.
 
Irina mwenye miaka 29 alituma ujumbe kuwa amejiondoa katika wafuasi wa Ronaldo katika mtandao wa Twite ambaye ni mpenzi wake wa miaka mitano.
Drama hiyo ilianza baada ya Irina kushindwa kuhudhuria sherehe za tuzo za Ballon d’Or mjini Zurich siku ya jumatatu.
 
Cristiano mwenye miaka 29 aliungana na mtoto wake wa kiume mwenye miaka minne, Cristiano Jr jukwaani  baada ya kupewa tuzo yake ya tatu ya mwanasoka bora wa dunia.
Katika hotuba yake aliishukuru familia yake, wachezaji wenzake na mashabiki wake, lakini hakumtaja mchumba wake Irina.
ronaldo split
Ronaldo na Irina mwaka 2011
Baadaye ripoti zilieleza kuwa mshambuliaji huyo wa Real Madrid amevunja mahusiano na mwanamitindo huyo wa Urusi baada ya kugoma kuacha kazi yake na kuwa mke na mama wa nyumbani.
 
Vyanzo vya karibu na mwanasoka huyo wa Ureno vimelieleza gazeti la Ureno la Correio da Manha kuwa mgogoro huo ulianzia kwenye sherehe ya kuzaliwa ya mama yake Ronaldo, Dolere wakati wapenzi hao walipokuwa katika mapumziko ya Krismas mjini Dubai.
 
Vyanzo vilisema: “Cristiano alitaka kumfanyia mama yake ‘sapraizi na alifurahia krismas na Irina huko Dubai, alipanga kuwa naye katika sherehe ya kuzaliwa ya mama yake, lakini Irina hakutaka kwenda”.
 
“Suala hilo lilileta mgogoro mkubwa na kusababisha kila mtu kufurahia sherehe za mwaka mpya peke yake na hawajawa na mahusiano mazuri miezi michache iliyopita”.
Gazeti hilo pia limedai kuwa Irina aliamua kukaa hotelini kwenye moja ya ziara zake Madrid kwasababu Doleres alipigwa picha akitoa machozi akiwa katika nyumba ya kifahari ya Ronaldo huko VIP estate La Finca kufuatia mwanaye kushinda tuzo ya tatu ya Ballon d’Or.
 
“Dolores anaamini Irina hakuwa mwanamke sahihi kwa mtoto wa Ronaldo,” vyanzo vililiambia gazeti la Correio da Manha.
Irina  na Cristiano, ambao walianza mahusiano baada ya kukutana Armani Photoshoot hawajathibitisha taarifa hizo rasmi za kuachana.
Msemaji wa Irina amedai kuwa mwanamitindo huyo alishindwa kuhudhuria Ballon d’Or kwasababu alikuwa na majukumu mengine
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: CRISTIANO RONALDO AACHANA NA MCHUMBA WAKE, KISA……………
CRISTIANO RONALDO AACHANA NA MCHUMBA WAKE, KISA……………
http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2015/01/ronaldo-552244.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2015/01/cristiano-ronaldo-aachana-na-mchumba.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2015/01/cristiano-ronaldo-aachana-na-mchumba.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy