Serikali imetenga Bil 9 ukarabati wa mji mkongwe :Rais Mwinyi
HomeHabariTop Stories

Serikali imetenga Bil 9 ukarabati wa mji mkongwe :Rais Mwinyi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ameeleza Serikali imetenga jumla ya shilingi Bilioni 9 kwa aji...

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ameeleza Serikali imetenga jumla ya shilingi Bilioni 9 kwa ajili ya kufanya ukarabati mkubwa wa majengo yaliyo katika hali mbaya zaidi ndani ya Mji Mkongwe ambayo wananchi hawamudu gharama za kukarabati.

Rais Dk. Mwinyi amesema hayo leo tarehe 2 Disemba 2024 kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Mji Mkongwe wa Zanzibar yaliyofanyika katika viwanja vya bustani ya Forodhani, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Rais Dk. Mwinyi ametumia maadhimisho hayo kuishukuru Serikali ya Oman kwa kuungamkono kwa hali na mali juhudi za Zanzibar za kuuhifadhi Mji Mkongwe na maeneo mengine ya kihistoria yaliopo Zanzibar kwani msaada huo umechangia kuyaweka maeneo hayo kuwa endelevu wakati wote.

Aidha, Dk. Mwinyi amezipongeza Kampuni za Infinity, Maxbit na Tume ya Taifa ya UNESCO ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mchango mkubwa wanaoutoa kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa Mamlaka ya Mji Mkongwe.

Rais Dk. Mwinyi amesifu hatua ya Mamlaka ya Mji Mkongwe kwa kuanzisha Mfumo wa kiditali aliouzindua katika kilele cha siku hiyo kwa uendeshaji wa mamlaka hiyo na usimamizi wa uingiaji wa watalii hatua itakayochangia kuongoza mapato ya Serikali na utoaji wa taarifa sahihi za Mji Mkongwe.

Waziri wa Utalii na mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga amesema  mabadiliko chanya uongozi wa Serikali ya awamu ya nane yameleta mabadiliko makubwa kwa Mji Mkongwe na kuuongezea umaarufu zaidi kimataifa.

Naye, Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mji Mkongwe, Mhandisi Ali Said Bakari, ameishukuru Serikali ya Oman kwa msaada wa Dola za Kimarekani milioni 25 kwa ukarabati wa jengo la Beit el Ajaab ambalo lina umuhimu kwa historia na Utalii wa Zanzibar.

 

The post Serikali imetenga Bil 9 ukarabati wa mji mkongwe :Rais Mwinyi first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/CQRF0lZ
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Serikali imetenga Bil 9 ukarabati wa mji mkongwe :Rais Mwinyi
Serikali imetenga Bil 9 ukarabati wa mji mkongwe :Rais Mwinyi
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2024/12/IMG-20241203-WA0029-950x633.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2024/12/serikali-imetenga-bil-9-ukarabati-wa.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2024/12/serikali-imetenga-bil-9-ukarabati-wa.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy