Mwinyi “Tutashirikiana na sekta binafsi kufikia malengo ya afya”
HomeHabariTop Stories

Mwinyi “Tutashirikiana na sekta binafsi kufikia malengo ya afya”

Rais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi amesema wanahitaji kuimarisha ushirikiano sekta binafsi na washirika wa maendeleo ili kufikia malengo ya ...

Rais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi amesema wanahitaji kuimarisha ushirikiano sekta binafsi na washirika wa maendeleo ili kufikia malengo ya afya bora kwa wananchi wote na kuondosha changamoto zinazoikabili sekta hiyo.

Changamoto hizo ni kupunguza vifo vya mama na mtoto, upatikanaji wa dawa muhimu, uimarishaji wa miundombinu ya afya, upatikanaji wa taarifa za afya, udhibiti wa maradhi ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza na mengineyo.

Rais Mwinyi ametoa kauli hiyo leo Oktoba 3, 2024 wakati akifunga kongamano la 11 la Tanzania Health Summitt (THS) lililofanyika katika Ukumbi wa Zanzibar International Trade Fair Fumba Nyamanzi Unguja.

“Tunahitaji kuendelea kuimarisha ushirikiano wa karibu na mashirika ya kimataifa na washirika wa maendeleo, kwani tumeona jinsi inavyofanikisha utekelezaji wa miradi mikubwa na kuimarisha mifumo ya afya nchini,” amesema Dk Mwinyi

Amesema wameshuhudia mifano mbalimbali ya jinsi ubia huo unavyoweza kuleta matokeo chanya katika upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wananchi hasa huduma za afya katika ngazi ya kati.

Amesisitiza kuwa changamoto zote zilizojadiliwa zinahitaji kuchukuliwa hatua madhubuti na za haraka.

Amesema tathmini ya mkutano huu imeonesha mafanikio makubwa yaliyopatikana katika sekta ya afya kupitia ubunifu na matumizi ya teknolojia, kama vile programu za afya za kidigitali zinazosaidia kuimarisha huduma za afya na mifumo ya taarifa za afya.

Naye Rais wa THS Dk Omary Chillo amesema kongamano hili lilikuwa ni fursa muhimu ambapo wataalamu wa afya, viongozi wa Serikali, na wadau kutoka sekta binafsi wameungana na kubadilishana mawazo kuhusu mustakabali wa sekta ya afya nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Kwa upande mwingine THS ambao ndio waandaji wakuu wa Kongamano la 11 la Afya ‘Tanzania Health Summit’ (THS) wamewatunuku tuzo ya ushiriki, kutambua mchango wa Shirika lisilo la kiserikali la kupitia Mradi wa Afya-Tek kwa njia ya kidigitali kuboresha afya ya mama, mtoto pamoja na kijana balehe.

Tuzo hiyo imepokelewa na Mkuu wa Mradi wa Afya-Tek, Dk. Angel Dillip kwenye Kongamano la 11 la Afya ‘Tanzania Health Summit’ kujadili njia bunifu zitakazosaidia katika utoaji wa huduma bora za afya kwa umma.

Waziri wa Afya Zanzibar, Ahmed Mazrui amesema mkutano huo umeonyesha namna wanavyoweza kushirikiana na kupata mbinu tofauti za kushughulikia changamoto za afya

Ametumia fursa hiyo kuwataka wataalamu hao kufanya tafiti mbalimbali za afya kwani zimeonyesha zinavyoleta mabadiliko chanya na kupata ufumbuzi wa changamoto.

Kongamano hilo la 11, limefanyika kwa siku tatu na kuwashirikisha wataalamu kutoka ndani na nje ya nchi lengo ni kujadili na kutafuta suluhisho la matatizo yanayoikumba sekta ya afya.

Lilifunguliwa Oktoba Mosi na Rais Samia Suluhu Hassan aliyewakilishwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla aliyesoma hotuba yake kwa niaba.
Mwisho.

The post Mwinyi “Tutashirikiana na sekta binafsi kufikia malengo ya afya” first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/6gJj8Az
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Mwinyi “Tutashirikiana na sekta binafsi kufikia malengo ya afya”
Mwinyi “Tutashirikiana na sekta binafsi kufikia malengo ya afya”
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2024/10/IMG_0775-950x633.jpeg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2024/10/mwinyi-tutashirikiana-na-sekta-binafsi.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2024/10/mwinyi-tutashirikiana-na-sekta-binafsi.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy