HomeHabariTop Stories

Kim Jong Un aamuru maafisa 30 kunyongwa kwa kushindwa kuzuia vifo wakati wa mafuriko makubwa

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, ameripotiwa kuamuru kuuawa kwa maafisa wapatao 30 kufuatia kushindwa kwao kuzuia mafuriko makubwa ...

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, ameripotiwa kuamuru kuuawa kwa maafisa wapatao 30 kufuatia kushindwa kwao kuzuia mafuriko makubwa na maporomoko ya ardhi yaliyosababisha vifo vya watu takriban 1,000 mwezi Julai.

Kulingana na ripoti ya Chosun TV ya Korea Kusini , ilimnukuu kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un kutaka adhabu kali itolewe kwa wale wanaodaiwa kuhusika na hasara isiyokubalika ya maisha ya watu, iliyosababishwa na mafuriko ya hivi majuzi.

Mafuriko hayo, ambayo yaliharibu zaidi ya nyumba 4,000 na kuwahamisha wakazi 15,000, yalisababisha Kim Jong Un kutoa agizo la adhabu kali kwa maafisa waliohusika. Ingawa majina ya maafisa walionyongwa hayajatajwa, Shirika la Habari la Korea Kaskazini (KCNA) liliripoti kwamba Kang Bong-hoon, katibu wa Kamati ya Chama ya Mkoa wa Chagang tangu 2019, alikuwa miongoni mwa viongozi walioondolewa kwenye nyadhifa zao na Kim Jong- un.

Kim Jong Un pia alitembelea maeneo yaliyoathirika na mafuriko na kusema kuwa itachukua miezi kadhaa kujenga upya na kurejesha maeneo hayo. Serikali ilitoa makazi kwa watu 15,400 mjini Pyongyang, wakiwemo vikundi vya watu walio katika mazingira magumu kama vile watoto, wazee, na askari walemavu.

Hata hivyo, Kim alikanusha ripoti za vifo vingi kutokana na mafuriko hayo, akizitaja kama uvumi wa uongo uliosambazwa na Korea Kusini kama sehemu ya kampeni ya kuharibu sifa ya Korea Kaskazini kimataifa. Ripoti za hivi karibuni zinaonyesha kuwa idadi ya adhabu za kifo nchini Korea Kaskazini imeongezeka sana tangu janga la COVID-19, kutoka wastani wa 10 kwa mwaka kabla ya janga hadi takriban 100 kwa mwaka.

The post Kim Jong Un aamuru maafisa 30 kunyongwa kwa kushindwa kuzuia vifo wakati wa mafuriko makubwa first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/u23owdU
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Kim Jong Un aamuru maafisa 30 kunyongwa kwa kushindwa kuzuia vifo wakati wa mafuriko makubwa
Kim Jong Un aamuru maafisa 30 kunyongwa kwa kushindwa kuzuia vifo wakati wa mafuriko makubwa
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2024/09/kim-jong-un-aamuru-maafisa-30-kunyongwa.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2024/09/kim-jong-un-aamuru-maafisa-30-kunyongwa.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy