TASAC yapongezwa,usimamizi wa kanuni ya usalama wa mizigo na utendaji kazi wa bandari na bandari kavu
HomeHabariTop Stories

TASAC yapongezwa,usimamizi wa kanuni ya usalama wa mizigo na utendaji kazi wa bandari na bandari kavu

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo imeipongeza Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kwa kusimamia kanuni za usalama wa mizigo ...

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo imeipongeza Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kwa kusimamia kanuni za usalama wa mizigo na usalama wa utendaji kazi wa bandari na bandari kavu hapa nchini.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo, Mhe. Dkt.Jason Rweikiza (Mb) leo tarehe 02 Agosti,2024 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara ya kamati hiyo kutembelea TASAC.

 

“Sisi Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo tumefurahi na kuona udhibiti unaotolewa na TASAC katika kusimamia kanuni hiyo unatekelezwa na wadau vizuri,” alisema Mhe. Dkt. Rweikiza.

Kamati hiyo imefanya ziara ya kutembelea ofisi za TASAC zilizopo jengo la SUMATRA , Bandari kavu za PMM 2001 “Limited”, GALCO, TRH na gati namba 8 hadi 11 ya meli za makasha zinazohudumiwa na Tanzania East A frica Gateway Terminal Limited (TEAGL), gati namba 0 hadi 7 yanayoendeshwa DP World.

Aidha, Kamati imeweza kupokea maoni ya wadau wanaodhibitiwa na TASAC na kueleza kuwa TASAC wanafanya kazi vizuri na ni wasikivu wanapowasilisha changamoto zao kila zinapojitokeza.

 

“Inapotokea changamoto yoyote TASAC ukaa pamoja na sisi na kuitatua kwa haraka,” amesema Bw. Mathew Clift, Afisa Mkuu wa Fedha wa DP World.

Aidha, Bw. Clift amesema DP World kwa muda miezi minne tangu waanze kutoa huduma bandarini wameweza kuhudumia meli kwa wakati na kupelekea kupunguza muda wa meli kusubiri kuingia gatini kutoka siku 30 hadi siku 7 tu. Hali hii imepelekea kupunguza gharama kwa mlaji wa mwisho na kuongeza shehena na mapato ya nchi.

 

Naye Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe.David Kihenzile amesema kuwa kamati hiyo hupitia kanuni zinazosaidia utendaji kazi za udhibiti na kupelekea bandari kutoa huduma bora na salama katika bandari zetu.

“Leo Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo imefanya ziara ofisi za TASAC, Bandari kavu na hatimae Bandari ya Dar es Salaam. Katika ofisi za TASAC wamepitishwa kwenye wasilisho la Kanuni ya Ulinzi na Usalama wa Mizigo katika maeneo ya Bandari na Bandari kavu,” amesema Mhe. Kihenzile.

The post TASAC yapongezwa,usimamizi wa kanuni ya usalama wa mizigo na utendaji kazi wa bandari na bandari kavu first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/jeA7zTG
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: TASAC yapongezwa,usimamizi wa kanuni ya usalama wa mizigo na utendaji kazi wa bandari na bandari kavu
TASAC yapongezwa,usimamizi wa kanuni ya usalama wa mizigo na utendaji kazi wa bandari na bandari kavu
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2024/08/1-950x633.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2024/08/tasac-yapongezwausimamizi-wa-kanuni-ya.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2024/08/tasac-yapongezwausimamizi-wa-kanuni-ya.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy