Rais Samia aipongeza REA
HomeHabariTop Stories

Rais Samia aipongeza REA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameupongeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kazi nzuri wanazofan...

Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo November 28, 2024
Wadau wapongeza BOT kwa kudhibiti wanaokiuka taratibu za kifedha
Israel na Lebanon zafanya makubaliano ya kumaliza mzozo wa vita

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameupongeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kazi nzuri wanazofanya.

Mhe. Rais ametoa pongezi hizo leo Agosti 4 wilayani Kilombero, Mkoa wa Morogoro alipotembelea Kituo cha Kupokea na Kupoza umeme cha Ifakara kilichojengwa na Serikali ya Tanzania kupitia REA kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya kilichotatua changamoto ya muda mrefu ya umeme wa uhakika katika Wilaya ya Malinyi, Ulanga na Ifakara.

Awali akitoa maelezo kuhusu mradi huo, Naibu Waziri Nishati, Mhe. Judith Kapinga amesemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia kwa kuridhia kupitia Wizara ya Nishati kujenga vituo 75 vya kupokea, kupoza na kusambaza umeme ikiwa ni jitihada zake za kuhakikisha wananchi katika maeneo yote wanapata umeme wa uhakika.

“Kabla ya mwaka 2021 nchi ilikuwa ina vituo 61 tu vya kupokea na kupoza umeme, tunakushukuru sana Mhe. Rais kwa kuridhia ujenzi wa vituo vingine vipya 75.” Amesema Mhe. Kapinga

Mhe. Naibu Waziri Kapinga amesema kuwa, tayari vituo nane vimejengwa na kuanza kazi huku vituo sita vikifikia asilimia 97.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy amesema kituo cha Ifakara kimejengwa kutokana na uhitaji mkubwa wa umeme wilayani Ifakara, Malinyi na Ulanga na hii pia inatokana na shughuli kubwa za kilimo na uchimbaji madini.

Mhandisi Hassan ameongeza kuwa, kabla ya ujenzi kituo cha Ifakara umeme kwa mwezi ulikuwa ukikatika mara 18 ambapo hivi sasa ikitokea umeme umekatika basi ni mara moja.

Ameongeza kuwa gharama ya ujenzi wa kituo hicho ilikuwa ni shilingi bilioni 24.5 ambapo serikali imechangia gharama hizo pamoja na wadau wa maendeleo ambao ni Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) na kukamilika kwa kituo hicho haujasaidia tuu kuongeza thamani ya mazao bali pia umesaidia kuboresha huduma za kijamii kama afya kwa upatikanaji wa umeme wa uhakika katika hospitali na zahanati.

   

The post Rais Samia aipongeza REA first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/1LsGCbk
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Rais Samia aipongeza REA
Rais Samia aipongeza REA
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2024/08/1ce68f13-b5db-4c38-8234-a872114db4d0-950x633.jpeg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2024/08/rais-samia-aipongeza-rea.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2024/08/rais-samia-aipongeza-rea.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy