Mgodi wa GGM  waanza kutumia umeme wa gridi badala ya mafuta
HomeHabariTop Stories

Mgodi wa GGM waanza kutumia umeme wa gridi badala ya mafuta

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amezindua kituo cha kupokea na kupoza umeme katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (...

Habari kubwa Magazetini Kenya leo February 7, 2025
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo February 7, 2025
Endeleeni kutoa elimu ya chanjo kwa akina mama pamoja na elimu ya mabagi

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amezindua kituo cha kupokea na kupoza umeme katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) chenye uwezo wa megawati 34 ambacho sasa kinawezesha GGML kuanza kutumia umeme wa gridi kwa matumizi yake badala ya mafuta na hivyo kupunguza gharama za uendeshaji.

Baada ya kuzindua kituo hicho tarehe 13 Agosti 2024 wilayani Geita mkoani Geita, Dkt.Biteko amesema ujenzi wa kituo hicho ni alama halisi ya umoja na ushirikiano uliopo kati ya Serikali na Sekta Binafsi kwani mradi huo umehusisha ujenzi wa laini ya umeme ya kV 33 ambayo imejengwa na TANESCO kwa gharama ya shilingi bilioni 8.04 huku GGML ikijenga kituo cha kupoza umeme kwa gharama ya Dola za Marekani milioni 24.

Amesema GGM ilikuwa inatumia shilingi bilioni 130 kwa mwezi kama gharama za uendeshaji  na kwenye umeme wa mafuta ilikuwa inatumia shilingi bilioni 13.4 kila mwezi na kuathiri mapato yake kwa Serikali, hivyo kuanza kazi kwa kituo hicho kunapunguza gharama za uendeshaji kwa mgodi na kupelekea Serikali kuongeza mapato yake, kuongeza ajira na pia GGM kuweza kutanua shughuli zake.

Dkt.Biteko ameipongeza kampuni hiyo kwa kuanza kutumia umeme wa gridi ambao unapunguza gharama za uendeshaji ambapo ametoa angalizo kuwa, kupungua kwa gharama hizo kuguse pia watumishi kwa kuboresha maslahi yao.

Ameeleza kuwa, umeme mwingi unaozalishwa kwa sasa unatoa uhakika wa kwenda kwa wananchi na walaji wakubwa kama GGM na kuweka mkazo kuwa, hayo ni matokeo ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuijali sekta binafsi.

Vilevile, ameipongeza GGM kwa kuzipa kipaumbele kampuni za kizawa katika kutoa huduma kwenye mgodi huo na kusisitiza kuwa huo ndio msimamo wa Serikali ya Tanzania wa kuhakikisha kampuni za ndani zinapewa kipaumbele kwenye miradi mbalimbali.

Dkt. Biteko amewaagiza Watendaji wa Wizara ya Nishati, TANESCO na Taasisi nyingine za Serikali kujali sekta binafsi kutokana na manufaa yake ikiwemo kuwa walipakodi wakubwa na kuongeza ajira nchini.

Pia, amewashukuru watangulizi wake katika Sekta ya Nishati, Dkt. Medard Kalemani na January Makamba ambao katika kipindi chao wakihudumu kama Mawaziri wa Nishati waliusimamia mradi huo ipasavyo.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio amesema hali ya umeme nchini kwa ujumla ni nzuri huku uzalishaji ukikidhi mahitaji na ziada kidogo.

Kuhusu usambazaji umeme mkoani Geita amesema kuwa Mkoa una Vijiji 486 na kati ya hivyo vijiji 483 vina umeme sawa na asilimia 99.38.

Ameongeza kuwa, kazi ya kupeleka umeme vitongojini mkoani Geita inaendelea ambapo kati ya vitongoji 2,197, vitongoji takriban 1000 tayari vina umeme.

Ameongeza kuwa, Mkoa wa Geita umetengewa Shilingi  bilioni 8.5 kwa ajili ya kupeleka umeme maeneo ya migodi na viwanda na utekelezaji umefikia asilimia 41.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigella  amemshukuru Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji nchini ambayo yamepelekea wawekezaji kufanya kazi na kuletea nchi faida akitolea mfano kuwa,  katika kipindi cha miaka mitatu GGM imezalisha tani 51 za dhahabu ambayo ni mafanikio makubwa yanayochangia ukuaji wa pato la Taifa.

Amemshukuru Rais Samia kwa kuwezesha umeme kufika pia kwenye migodi  ya Wachimbaji wadogo ambapo katika kipindi cha miaka mitatu wachimbaji wadogo 19 wamepelekewa umeme kwenye migodi yao na kuwezesha uzalishaji wa kilo za dhahabu takriban 11,000.

The post Mgodi wa GGM waanza kutumia umeme wa gridi badala ya mafuta first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/fEjKrm7
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Mgodi wa GGM waanza kutumia umeme wa gridi badala ya mafuta
Mgodi wa GGM waanza kutumia umeme wa gridi badala ya mafuta
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2024/08/cf4b450a-75f0-4f91-890e-b5c2c9e8c8cc-950x485.jpeg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2024/08/mgodi-wa-ggm-waanza-kutumia-umeme-wa.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2024/08/mgodi-wa-ggm-waanza-kutumia-umeme-wa.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy