AU watambua jitihada za Rais Samia na Ulega kuwainua wavuvi
HomeHabariTop Stories

AU watambua jitihada za Rais Samia na Ulega kuwainua wavuvi

UMOJA wa Afrika (AU) na Shirika la Kilimo na Chakula (FAO) wamemtambua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na Wazir...

UMOJA wa Afrika (AU) na Shirika la Kilimo na Chakula (FAO) wamemtambua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, kama vinara wa kuwapambania wavuvi wadogo Afrika, ikiwa ni mwendelezo wa Mkutano wa Kimataifa wa wavuvi wadogo uliofanyika kwa siku mbili, Mlimani City, jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo umeshirikisha watu zaidi ya 1000 kutoka mataifa mbalimbali Barani Afrika, ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Naibu Waziri Mkuu, Dotto Biteko akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan na kushuhudia hoja mbalimbali zikijadiliwa kwa lengo la kuwaendeleza wavuvi wadogo nchini Tanzania.

Akizungumza katika Mkutano huo wa kwanza Barani Afrika mwakilishi wa umoja wa Mataifa AU-IBAR, Hellen Moepi-Guebama, alisema mkutano huu wa kwanza uliohusisha wavuvi wadogo na kushirikisha watu wa kutoka nchi mbalimbali barani Afrika, una lengo la kuangalia namna nzuri ya kuwakomboa wavuvi wadogo Afrika.

“Tunatambua mchango wa Rais Samia kuanzisha na kusaidia wavuvi wadogo haswa kwa namna ya kutafsiri sera, miongozo, kanuni, pamoja na mpango kazi wenye lengo la kuisaidia sekta hii muhimu ya uvuvi barani Afrika.

“Aidha Tanzania kwa kupitia jitihada za Rais Samia, tumeshuhudia mkutano mkubwa wa wavuvi wadogo wenye lengo la kukusanya maoni ya wavuvi yatakayokwenda kufanyiwa kazi katika Mkutano wa Kimataifa utakaofuata nchini Italia,” Alisema Hellen.

Naye Mwakilishi wa Shirika la Kilimo na Chakula FAO, nchini Tanzania, Dr Tipo Nyabenyi Tipo, alisema kufanyika kwa mafanikio kwa tukio la wavuvi wadogo ni juhudi madhubuti na malengo ya juu aliyokuwa nayo Rais Samia.

“Nchini Italia mwaka jana Waziri Ulega aliahidi Tanzania kuandaa mkutano huu, ambao leo tunaona umefanikiwa kwa asilimia kubwa. Haya ni matunda ya serikali ya Rais Samia ambapo tunaona ni mwendo mzuri katika sekta hii ya uvuvi mdogo,”Alisema Dr Tipo.

Nyabenyi alisema endapo sekta ya uvuvi mdogo itaendelezwa na kupewa ushirikiano, jamii itanufaika kwa sababu sekta hiyo inatumika pia kama chanzo cha mapato cha watu wengi.

Naye Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, aliwashukuru wadau wote kwa kushiriki mkutano huo, huku akisema kuwa kama Tanzania ina dhamira ya kuwainua wavuvi wadogo kwa kuhakikisha kuwa inafanyia kazi changamoto mbalimbali zinazowakabili ili sekta hiyo iwe na manufaa kwa wote, akisisitiza kuwa sekta ya uvuvi mdogo inahusisha asilimia 95 ya uvuvi wote nchini.

Katika Mkutano huo wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, maoni yanayotolewa na wadau yataenda kufanyiwa kazi katika Mkutano wa Kimataifa wa Uvuvi huko nchini Italia.

The post AU watambua jitihada za Rais Samia na Ulega kuwainua wavuvi first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/xoMwcWK
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: AU watambua jitihada za Rais Samia na Ulega kuwainua wavuvi
AU watambua jitihada za Rais Samia na Ulega kuwainua wavuvi
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2024/06/7df3496d-3569-4662-bb32-178df021bcce-950x539.jpeg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2024/06/au-watambua-jitihada-za-rais-samia-na.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2024/06/au-watambua-jitihada-za-rais-samia-na.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy