Wakuu Wa Nchi Za EAC Wasisitiza Umuhimu Wa Soko La Pamoja Katika Kukuza Uchumi Wa Kikanda
HomeHabari

Wakuu Wa Nchi Za EAC Wasisitiza Umuhimu Wa Soko La Pamoja Katika Kukuza Uchumi Wa Kikanda

  Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wamesisitiza umuhimu wa soko la pamoja katika kukuza uchumi wakati waliposhiriki Mku...

Dkt.Ndumbaro Ataja Manufaa Ya Fedha Za Mkopo Kwa Wananchi Wa Mkoa Wa Ruvuma
CCM Wasema Yanayofanywa Na Rais Samia Yanabaraka Zote Za Chama
Spika Ndugai Atoa Ufafanuzi Kuhusu Hotuba Yake Iliyozua Taharuki


 Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wamesisitiza umuhimu wa soko la pamoja katika kukuza uchumi wakati waliposhiriki Mkutano Maalum wa Ngazi ya Juu wa Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mkutano huo maalum wa ngazi ya Wakuu wa Nchi uliofanyika tarehe 21 Julai 2022 na mkutano maalum wa ngazi ya Mawaziri uliofanyika tarehe 20 Julai 2022 jijini Arusha ni sehemu ya mikutano ya awali kuelekea Mkutano wa 22 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika tarehe 22 Julai 2022.

Katika mkutano huo Wakuu wa Nchi walijadili na kuyawekea msisitizo masuala mbalimbali ya hali ya halisi ya utekelezaji wa Itifaki ya Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki sambamba na kuainisha changamoto zinazohitaji ufumbuzi wa pamoja katika kuyafikia malengo ya jumuiya hiyo.

Akichangia mada wakati wa mkutano huo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni mwenyeji wa mkutano huo, amesisitiza juu ya kukuza uzalishaji pamoja na kuongeza thamani ya mazao na bidhaa zinazozalishwa ndani ya jumuiya ili kuweza kuingia katika ushindani wa kibiashara kimataifa.

Aidha, aliongeza kufafanua kuwa katika kuyafikia malengo ya pamoja ni muhimu kwa nchi wanachama kuwekeza katika amani na utawala bora ili nchi ziweze kuongeza nguvu katika usimamizi wa rasilimali na uzalishaji badala ya kuwekeza katika migogoro.

Naye Mwenyekiti wa mkutano huo na Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Uhuru Kenyatta amesisitiza umuhimu wa kuwa na mawasiliano kupitia ujenzi wa miundombinu ambao ndio msingi mkuu wa kuyafikia malengo ya soko la pamoja.

Vilevile akaeleza kwa sasa nchi wanachama zimeunganishwa kupitia ujenzi wa miundombinu ya kisasa na akatolea mfano ujenzi wa reli ya kisasa unaofanywa na Tanzania ambao utaziunganisha nchi wanachama na kwamba kwa upande mwingine Tanzania na Kenya zinaunganishwa kupitia ujenzi wa miundombinu uliofanywa mipakani katika eneo la Namanga na Taveta.

Maeneo mengine yaliyojadiliwa ni pamoja na fursa za kiuchumi zilizoongezeka kufuatia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kujiunga na jumuiya hiyo, umuhimu wa usimamizi wa rasilimali kama vile madini na umuhimu wa ushiriki wa sekta binafsi katika kuyafikia malengo yaliyowekwa.

Kadhalika, mkutano huo ulijadili mafanikio yaliyofikiwa na jumuiya hiyo ikiwemo, uhuru wa kufanya biashara, mtangamano wa kijamii na fursa za kuvuka mipaka kupitia Hati ya kusafiria ya kielektroni ya Afrika Mashariki na kuondoleana visa miongozi mwa nchi wanachama.

Mkutano huo umehudhuriwa na Nchi zote saba wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao ni pamoja mwenyekiti wa mkutano huo Jamhuri ya Kenya; Mwenyeji wa mkutano huo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Jamhuri ya Uganda; Jamhuri ya Burundi, Jamhuri ya Rwanda, Jamhuri ya Sudan Kusini, na Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo. Pia ulihudhuriwa na Jamhuri ya Shirikisho la Somalia ambaye alikuwa mgeni mwalikwa katika mkutano huo



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Wakuu Wa Nchi Za EAC Wasisitiza Umuhimu Wa Soko La Pamoja Katika Kukuza Uchumi Wa Kikanda
Wakuu Wa Nchi Za EAC Wasisitiza Umuhimu Wa Soko La Pamoja Katika Kukuza Uchumi Wa Kikanda
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi0OwNIlpqYmoHcmXEkkIIBs1EqX1a9h6eQCK0-pSn-l1RR0BrrmccHfsNTW0VV66Z2rMt8lpn0Dq3MDne59o-bsOHIjIQMYedKvVXwblNC7kUs9PO50MsYNRPICT-Zjvp_SdHiy0PO3X5ZYaV31jUoi854QFFK4nuoznmaxIIuwX_vRnzqNWOh1KsFzQ/s16000/WhatsApp%20Image%202022-07-22%20at%2012.29.07%20AM.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi0OwNIlpqYmoHcmXEkkIIBs1EqX1a9h6eQCK0-pSn-l1RR0BrrmccHfsNTW0VV66Z2rMt8lpn0Dq3MDne59o-bsOHIjIQMYedKvVXwblNC7kUs9PO50MsYNRPICT-Zjvp_SdHiy0PO3X5ZYaV31jUoi854QFFK4nuoznmaxIIuwX_vRnzqNWOh1KsFzQ/s72-c/WhatsApp%20Image%202022-07-22%20at%2012.29.07%20AM.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/07/wakuu-wa-nchi-za-eac-wasisitiza-umuhimu.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/07/wakuu-wa-nchi-za-eac-wasisitiza-umuhimu.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy