Ofisi Ya Wakili Mkuu Wa Serikali Yaanza Ujenzi Wa Ofisi Katika Mji Wa Serikali Mtumba, Dodoma
HomeHabari

Ofisi Ya Wakili Mkuu Wa Serikali Yaanza Ujenzi Wa Ofisi Katika Mji Wa Serikali Mtumba, Dodoma

Na Prisca Ulomi, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Dodoma Wawakilishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali (OWMS) wakiongozwa na Naibu Wa...

Waziri Mkuu Majaliwa Asema Serikali Inajipanga Kukarabati Nyumba Za Walimu....Afurahishwa Na Ubunifu Wa Wanafunzi Wa Shule Ya Sekondari Ya Ufundi Ifunda
Rais wa Ethiopia kufanya ziara nchini
Serikali Yaingia Makubaliano Na Wafanyabiashara Ya Ngano


Na Prisca Ulomi, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Dodoma

Wawakilishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali (OWMS) wakiongozwa na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Boniphace Luhende leo tarehe 18 Juni, 2022 wameshuhudia makabidhiano ya eneo la ujenzi wa Ofisi za Makao Makuu ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali lenye ukubwa wa mita za mraba 17,342.

Makabidhiano hayo yamefanyika kwenye Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma baina ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ambaye ni Mshauri Elekezi aliyewakilishwa na Msanifu Majengo Weja Ng’olo na Kampuni ya Ujenzi ya SUMA JKT ambae ni Mkandarasi iliyowakilishwa na Mkadiriaji Majenzi, Jacob Ghati.

Akikabidhi eneo hilo, Mwakilishi wa TBA, Ng’olo ameeleza kuwa jengo la Ofisi linalotarajiwa kujengwa ni la kisasa na ni miongoni mwa majengo yenye muonekano mzuri katika Mji wa Serikali Mtumba. Jengo hili litakuwa na miundombinu mbalimbali ikiwemo vyumba vya Ofisi 127, maegesho ya magari 111, maktaba, kumbi 2 za mikutano zenye nafasi 108 kila mmoja, kumbi 2 za kutolea mafunzo zenye nafasi 42 kila mmoja, maabara ya kompyuta, vyumba vidogo 10 vya mikutano na chumba cha akina mama wanyonyeshao.

Ujenzi wa jengo hilo unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi kumi na nane (18).

Akizungumza kwa niaba ya Mkandarasi, Gati amesema kuwa wako tayari kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwa mujibu wa mkataba na kwa kushirikiana na Mshauri Elekezi (TBA) na Mshitiri (OWMS).

Kwa upande wake, Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Luhende amewatakia Mkandarasi na Mshauri Elekezi utekelezaji mwema wa majukumu yao kwa mujibu wa mkataba na kwa kuzingatia weledi.

Pia amewahakikishia kuwa Ofisi ya Wakili Mkuu Serikali itawapa ushirikiano unaostahili.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,

Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Ofisi Ya Wakili Mkuu Wa Serikali Yaanza Ujenzi Wa Ofisi Katika Mji Wa Serikali Mtumba, Dodoma
Ofisi Ya Wakili Mkuu Wa Serikali Yaanza Ujenzi Wa Ofisi Katika Mji Wa Serikali Mtumba, Dodoma
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjwWsKIeGdCGtDRth4NX-5oEvd0u-AzdLo1JFNS4ElwKOUPQIxirEE6zmCLKhnVLtAG26kQkcD5k9vsbBS8FQYbeIAb35nApLSMGSOZ2wJH43H3AJjotb__P7SosiEeZt1RbgJvBfnTGR-1vSzRAyZN_eoS9rvu3rRk5sYi90Q4Q8uun78_T-79UOzjxQ/s16000/WhatsApp-Image-2022-06-20-at-4.44.29-PM-2.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjwWsKIeGdCGtDRth4NX-5oEvd0u-AzdLo1JFNS4ElwKOUPQIxirEE6zmCLKhnVLtAG26kQkcD5k9vsbBS8FQYbeIAb35nApLSMGSOZ2wJH43H3AJjotb__P7SosiEeZt1RbgJvBfnTGR-1vSzRAyZN_eoS9rvu3rRk5sYi90Q4Q8uun78_T-79UOzjxQ/s72-c/WhatsApp-Image-2022-06-20-at-4.44.29-PM-2.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/06/ofisi-ya-wakili-mkuu-wa-serikali-yaanza.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/06/ofisi-ya-wakili-mkuu-wa-serikali-yaanza.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy