Waziri Mulamula Amwakilisha Rais Samia Mkutano Wa Dharura AU
HomeHabari

Waziri Mulamula Amwakilisha Rais Samia Mkutano Wa Dharura AU

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tan...

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo May 22
Uteuzi Wa Wajumbe Wa Bodi Ya Taasisi Ya Uhandisi Na Ubunifu Mitambo Tanzania TEMDO
RC Makalla amaliza ugomvi wa Meya na Mkurugenzi Kinondoni


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa 15 wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) unaofanyika Malabo, Equatorial Guinea tarehe 27 na 28 Mei, 2022.

Mkutano huo pamoja na mambo mengine, umejadili ajenda kuu mbili ambazo ni majanga na huduma za kibinadamu, masuala ya Ugaidi na Mabadiliko ya Serikali yasiyozingatia misingi ya Katiba. 

Akiongea wakati wa Mkutano huo, Balozi Mulamula amesema anamwakilisha Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan katika Mkutano huo ulioitishwa na na Umoja wa Afrika (AU) kwa lengo la kuangalia na kujadili maajanga na huduma za kibinadamu pamoja na ugaidi.

“AU wameitisha mkutano huu kwa lengo la kujadili namna ya kukabiliana na majanga haya na jinsi gani Bara la Afrika linaweza kuwa na mkakati wa pamoja wa kukabiliana na majanga haya, na tunategemea baada ya kikao cha leo tutapata azimio la kukabidiliana na majanga haya katika bara letu la Afrika,” amesema Balozi Mulamula.

Kuhusu masuala ya Ugaidi, Balozi Mulamula ameongeza kuwa, Mkutano wa  tarehe 28 Mei, 2022 mkutano utaendelea kuangalia masuala ya kigaidi na kuona ni jinsi gani Bara la Afrika linasimama kwa umoja wake kupambana na majanga ya kigaidi.

Awali akifungua Mkutano huo, Rais wa Senegali ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mkutano huo, Mhe. Macky Sall amezisihi nchi za Afrika kuwa na umoja ambao utaziwezesha kukabiliana na majanga ya kibinadamu na mapambano dhidi ya ugaidi kwa urahisi zaidi.

Mhe. Sall amezitaka nchi za Afrika kuimarisha ushirikiano na mshikamano na kujenga uwezo wa kila nchi ili kuweza kukabiliana na majanga mbalimbali ya asili na wakati huo huo, kushughulikia changamoto za ulinzi na usalama ili kutozalisha wakimbizi na wahamaji ikiwa ni pamoja na kuimarisha ushirikiano na kuunda Jeshi la Afrika (ASF) na Brigedi za kikanda pamoja na kuanzisha Vikosi Maalum    kushughulikia Changamoto za Ugaidi.

Balozi Mulamula katika mkutano huo, ameambatana na Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Mhe. Innocent Shiyo ambaye anawakilisha pia Umoja wa Afrika, Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Naimi Aziz pamoja na watumishi wengine waandamizi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Waziri Mulamula Amwakilisha Rais Samia Mkutano Wa Dharura AU
Waziri Mulamula Amwakilisha Rais Samia Mkutano Wa Dharura AU
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj2zfcQ_39STxfxxtorprYwmU0r6UhLTqS9H_VxM0KVlrmZrhlKf5Peo8ZV-01b6mKtr_usoaCKRkK_P7dXtwuw0o_lHp53qoEeGqxKugOCTr3cYMqrSLfBPbIxgOw5DQcrwr4gpUXh4pmDx0NTXyepTOyGZJVMOUEbisldpOEkUARBVjt3-nJOzEJ2Dg/w640-h478/unnamed.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj2zfcQ_39STxfxxtorprYwmU0r6UhLTqS9H_VxM0KVlrmZrhlKf5Peo8ZV-01b6mKtr_usoaCKRkK_P7dXtwuw0o_lHp53qoEeGqxKugOCTr3cYMqrSLfBPbIxgOw5DQcrwr4gpUXh4pmDx0NTXyepTOyGZJVMOUEbisldpOEkUARBVjt3-nJOzEJ2Dg/s72-w640-c-h478/unnamed.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/05/waziri-mulamula-amwakilisha-rais-samia.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/05/waziri-mulamula-amwakilisha-rais-samia.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy