Waziri Mkuu Atoa Agizo Kwa Wanafunzi Waliorudishwa Nchini
HomeHabari

Waziri Mkuu Atoa Agizo Kwa Wanafunzi Waliorudishwa Nchini

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wanafunzi waliokuwa wanasoma katika vyuo mbalimbali nje ya nchi ambao walirudishwa nchini kufuatia k...

Escrow yauma vigogo BoT, TRA
Pentagon to deploy 400 troops to train Syrian rebels
Waisilamu waandamana dhidi ya C.Hebdo

 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wanafunzi waliokuwa wanasoma katika vyuo mbalimbali nje ya nchi ambao walirudishwa nchini kufuatia kuzuka kwa janga la UVIKO19 pamoja na kuibuka kwa vita kati ya Urusi na Ukraine wawasilishe taarifa zao Kamisheni ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).

Ametoa wito huo leo (Alhamisi, Mei 12, 2022) wakati akijibu swali la Mbunge wa Hai, Saasisha Mafuwe katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu. Mbunge


huyo alitaka kujua Serikali ina mpango gani wa kuwasaidia wanafunzi hao kuendelea na masomo wakiwa hapa nchini.

Waziri Mkuu amesema ili kuhakikishia wanafunzi hao wanasaidiwa kumaliza masomo yao wakiwa hapa nchini, Serikali inawataka wawasilishe taarifa zao TCU ambayo imeweka utaratibu unaoruhusu wanafunzi hao kuhamisha viwango vya ufaulu wa masomo vitakavyowawezesha kuendelea na masomo yao nchini.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu ametoa wito kwa Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kununua viuadudu kwa ajili ya kupuliza katika maeneo mbalimbali na kutokomeza mazalia na mbu wanaoambukiza ugonjwa wa malaria. Dawa hizo zinatengenezwa na  kiwanda cha Kibaha Tanzania Biotech Product Limited.

Mheshimiwa Majaliwa ametoa agizo hilo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Rose Tweve ambaye amesema Serikali ilifanya uwekezaji mkubwa wa katika kujenga kiwanda cha viuadudu kwa gharama ya wastani wa bilioni 46.

“Wizara ya Afya iliingia mkataba wa kununua dawa hizo na haikufanya kama ilivyokubalika. Je Serikali haioni umuhimu wa kuingia mkataba mpya na kiwanda hiki ili kuweza kununua dawa zitakazo saidia kutokomeza malaria nchini?” amehoji.

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema kwamba suala la ukarabati wa miundombinu mbalimbali katika shule kongwe nchini ni endelevu na kila mwaka Serikali inatenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa zoezi hilo.

Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa jimbo la Mwanga, Anania Thadayo aliyetaka kufahamu Serikali ina mpango gani wa dharura wa kuzifanyia ukarabati shule nyingi ambazo ilizozijenga kwa kipindi kirefu huku baadhi yake zimeanza kuchakaa.





Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Waziri Mkuu Atoa Agizo Kwa Wanafunzi Waliorudishwa Nchini
Waziri Mkuu Atoa Agizo Kwa Wanafunzi Waliorudishwa Nchini
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEirk6j8EDQnjCP0dg-HxxZqOerFLmfxT9VaBt-q4pripe9qcoaH2DRYw0dokl8l5GomLSHq91bl-o1-iFPZQLDMlwgavMLq3-BCskpThtH8z3ATcN0_ijuRWgB5KleNXoBAK_4PxBgndyDYpSfrb1pbJnMHjouQYE6SlXuX3lvhfjDeG551Z3UzKFgC9Q/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEirk6j8EDQnjCP0dg-HxxZqOerFLmfxT9VaBt-q4pripe9qcoaH2DRYw0dokl8l5GomLSHq91bl-o1-iFPZQLDMlwgavMLq3-BCskpThtH8z3ATcN0_ijuRWgB5KleNXoBAK_4PxBgndyDYpSfrb1pbJnMHjouQYE6SlXuX3lvhfjDeG551Z3UzKFgC9Q/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/05/waziri-mkuu-atoa-agizo-kwa-wanafunzi.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/05/waziri-mkuu-atoa-agizo-kwa-wanafunzi.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy