Kamati Ya Kitaifa Ya Kuzuia Mauaji Ya Kimbari Yajadili Mfumo Wa Kuzuia Migogoro Nchini
HomeHabari

Kamati Ya Kitaifa Ya Kuzuia Mauaji Ya Kimbari Yajadili Mfumo Wa Kuzuia Migogoro Nchini

 Na Mwandishi wetu, Dar es salaam Kamati ya Kitaifa ya Kuzuia Mauaji ya Kimbari imekutana Jijini Dar es Salaam kujadili uanzishwaji wa ...

IGP Sirro Awaasa Askari Kuheshimu Nafasi Waliyopewa
Rasmi Tanzania Mwenyeji Tuzo Za (MAMA) MTV AFRICA Music Award 2023
Serikali Yawasilisha Muswada Wa Sheria Ya Fedha Wa Mwaka 2022 Bungeni


 Na Mwandishi wetu, Dar es salaam

Kamati ya Kitaifa ya Kuzuia Mauaji ya Kimbari imekutana Jijini Dar es Salaam kujadili uanzishwaji wa Mfumo wa kuzuia migogoro nchini ili kurahisisha shughuli za uratibu wa kamati hiyo.

Akifungua kikao cha kamati hiyo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. George Simbachawene amepongeza kuanzishwa kwa mfumo huo hapa nchini ambao utasaidia kutambua dalili za awali  katika matukio yanayoweza kusababisha kutokea mauaji ya kimbari.

“Naishukuru UNDP kwa kubuni wazo la kuanzishwa kwa mfumo huo, kwani kutambua dalili za awali za matukio yanayoweza kusababisha  kutokea kwa mauaji ya kimbari kutasaidia sana kuepusha kutokea kwa mauaji hayo siyo tu hapa nchini bali hata kwa nchi nyingine wanachama wa jumuiya yetu, ni wazo zuri na wadau wamelipokea vizuri,” amesema Mhe. Simbachawene.

Amesema Serikali inaendelea na taratibu za kuanzisha ofisi kwa ajili ya kuratibu mauaji ya kimbari hapa nchini kwa ajili ya kusaidia harakati za kuzuia kutokea kwa mauaji ya kimbari kupitia mfumo huo.

Kwa Upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula ameipongeza Kamati ya Kitaifa ya Kuzuia Mauaji ya Kimbari ambayo imekuwa ikichukua hatua za kuwakutanisha wadau  mbalimbali katika jamii kama viongozi wa dini na jumuiya mbalimbali ili kutatua changamoto pale zinapotokea katika jamii nchini.

“Mimi kama mlezi wa kamati nimefarijika kuiona kamati hii ikitekeleza majukumu yake kwa ufanisi na siyo tu kuisaidia Tanzania bali hata nchi nyingine katika ukanda wa maziwa makuu,” amesema Balozi Mulamula.

Balozi Mulamula amepongeza Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa kushirikiana na Serikali ya Uswisi kwa  kuona umuhimu wa Kamati ya Kitaifa ya Kuzuia Mauaji ya Kimbari na hivyo kwa pamoja kuja na mpango wa kuanzishwa kwa kituo ambacho kitakuwa kinatoa taarifa za awali pale vinapokuwepo viashira vya matatizo au hata mauaji ya kimbari na kuongeza kuwa Serikali inaunga mkono jitihada hizo kwani zitaiwezesha kuzuia migogogo ambayo inaweza kusababisha kutokea mauaji  ya kimbari nchini.
 
Kamati ya Kitaifa ya Kuzuia Mauaji ya Kimbari nchini iliundwa mwezi Februari, 2012 baada ya Tanzania kusaini na kuridhia Itifaki ya Kuzuia Mauaji ya Kimbari iliyoridhiwa na Serikali ya Tanzania kupitia Mkataba wa nchi za Maziwa Makuu wa Usalama, Utulivu na Maendeleo.


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Kamati Ya Kitaifa Ya Kuzuia Mauaji Ya Kimbari Yajadili Mfumo Wa Kuzuia Migogoro Nchini
Kamati Ya Kitaifa Ya Kuzuia Mauaji Ya Kimbari Yajadili Mfumo Wa Kuzuia Migogoro Nchini
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEijtTOEeU9brSUHAcjjJCExkxEl8cbwY_chTkQMsqj9XDD6Bp4IzJ14LkIwM0IyWtUdcfc4RCeDQc3qzlZ_Cc9VYFNRozSjlAQmfUgRKPBEYjykLnXeoV4NHkEgTaL6NadCJzgS8VeiIaTPdgNnsyLI6l85lYJl8PzXZSMjvUS13UecE5fx6cGcu2Ne0A/s16000/1.jpeg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEijtTOEeU9brSUHAcjjJCExkxEl8cbwY_chTkQMsqj9XDD6Bp4IzJ14LkIwM0IyWtUdcfc4RCeDQc3qzlZ_Cc9VYFNRozSjlAQmfUgRKPBEYjykLnXeoV4NHkEgTaL6NadCJzgS8VeiIaTPdgNnsyLI6l85lYJl8PzXZSMjvUS13UecE5fx6cGcu2Ne0A/s72-c/1.jpeg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/03/kamati-ya-kitaifa-ya-kuzuia-mauaji-ya.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/03/kamati-ya-kitaifa-ya-kuzuia-mauaji-ya.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy