Dkt. Nchemba Ateta Na Chama Cha Watoa Huduma Za Simu Tanzania
HomeHabari

Dkt. Nchemba Ateta Na Chama Cha Watoa Huduma Za Simu Tanzania

 Saidina Msangi na Peter Haule, WFM-Dodoma Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) amekihakikishia Chama cha Wa...

 Saidina Msangi na Peter Haule, WFM-Dodoma


Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) amekihakikishia Chama cha Watoa Huduma za Simu Tanzania (TAMNOA) kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri ya biashara yatakayo iwezesha Sekta Binafsi kukua na kuchangia ukuaji wa uchumi wa Taifa.

Mhe. Nchemba alisema hayo jijini Dodoma alipokutana na kuzungumza na Chama cha Watoa Huduma wa Simu Tanzania (TAMNOA), wakati kikiwasilisha Serikalini maoni yao kuhusu sera za kodi ikiwa ni maandalizi ya Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/23.

“Sekta binafsi ikinawiri na Serikali inanawiri! Kwa sababu sekta binafsi ndiyo injini ya kuwezesha ukuaji wa uchumi wetu, kwa hiyo niwashukuru kwa maoni mliyotoa yakiwemo ya kutoza kodi maeneo yenye kipato kikubwa na kutoa msamaha wa kodi kwa wale wenye kipato kidogo ili kupunguza pengo la walio nacho na wasio nacho”, alisema Dkt. Nchemba.

Dkt. Nchemba alisema kuwa dira ya Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni kuona sekta binafsi inafanya kazi kwa mafanikio makubwa, kwa kuwa ni injini ya kukua kwa uchumi wetu, chanzo cha ajira kwa vijana lakini pia ni chanzo cha mapato kwa Serikali, hivyo ikikua na mapato ya Serikali yatakua.

Alisema kama Wizara imepokea maoni hayo na itasimamia utekelezaji wake ili kuangalia mianya mipya ya kutoza kodi hususani kampuni kubwa duniani zinazofanya biashara kwa njia ya kidijiti kwa kuweka sheria ili kodi hizo ziweze kutumika kutoa huduma kwa wananchi.

Aliwaelekeza wataalamu wa Wizara hiyo kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kupitia mapendekezo yaliyotolewa na wadau hao ili kuona namna bora ya kuyatumia mapendekezo hayo.

Aidha, Waziri Nchemba alitoa wito kwa wadau wengine ikiwemo Sekta binafsi nchini kuwasilisha mapendekezo na maoni yao mapema kuelekea maandalizi ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ili kuwa na sera za kikodi rafiki kwa ajili ya kuharakisha maendeleo ya nchi.

Alisema kuwa maoni na mapendekezo kutoka sekta binafsi ni muhimu katika kusaidia maboresho ya sera za kiuchumi na sera za kikodi ili kujenga mazingira rafiki kwa sekta binafsi nchini.

Kwa upande wake, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye, alisema kuwa mawazo yaliyotolewa na wadau ni mazuri na kuwa Serikali imeyachukua na yatafanyiwa kazi na kuiomba Wizara ya Fedha kuchambua maoni hayo mapema na kuwashirikisha wadau kuhusu maamuzi yatakayofikiwa.

Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali, alisema kuwa suala la kuangalia namna ya kuzitoza kodi kampuni kubwa duniani zinazofanya biashara kwa njia ya mtandao ni muhimu kwa kuwa yanakusanya fedha nyingi kutoka kwa wananchi lakini haziachi chochote kwa ajili ya maendeleo yao.

Kwa upende wao Chama cha Watoa Huduma za Simu Tanzania (TAMNOA) walisema kuwa mapendekezo waliyoyatoa yakifanyiwa kazi na kuanza utekelezaji wake mapato ya Serikali yataongezeka kutoka asilimia 61 hadi asilimia 64.9.


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Dkt. Nchemba Ateta Na Chama Cha Watoa Huduma Za Simu Tanzania
Dkt. Nchemba Ateta Na Chama Cha Watoa Huduma Za Simu Tanzania
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEifZdbplB30noeWHydDjpaMEgBuyo-SqU0LrN7dR956pPcxxZBe9Nllu-XWabXJKWKb10WZIRtH2igI-H7z95wRlpgNgPeIzDUqSsVfRId8vP6-g4DzOW4wWJYf5vEAm136kTyeU-9Tsmi-kJNsHoXjjLA6_7xKMFc8djQIR_0Yu8-FxFQTE8XpkcJ5MQ=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEifZdbplB30noeWHydDjpaMEgBuyo-SqU0LrN7dR956pPcxxZBe9Nllu-XWabXJKWKb10WZIRtH2igI-H7z95wRlpgNgPeIzDUqSsVfRId8vP6-g4DzOW4wWJYf5vEAm136kTyeU-9Tsmi-kJNsHoXjjLA6_7xKMFc8djQIR_0Yu8-FxFQTE8XpkcJ5MQ=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/02/dkt-nchemba-ateta-na-chama-cha-watoa.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/02/dkt-nchemba-ateta-na-chama-cha-watoa.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy