Tanzania Itaendelea Kushiriki Kikamilifu Kutekeleza Mkataba Wa AfCFTA
HomeHabari

Tanzania Itaendelea Kushiriki Kikamilifu Kutekeleza Mkataba Wa AfCFTA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Prof. Godius Kahyarara amesema Tanzania itaendelea kushirikiana na Sekretarieti y...


Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Prof. Godius Kahyarara amesema Tanzania itaendelea kushirikiana na Sekretarieti ya Eneo Huru la Biashara Afrika AfCFTA, Sekta Binafsi na Wadau wengine nchini kuwaelimisha wananchi kuchangamkia fursa za biashara na uwekezaji zinazopatikana katika Eneo  hilo.

Katibu Mkuu ameyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na  Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya AfCFTA
Mhe. Wamkele Mene Januari 24, 2022 katika Ofisi za Makao Makuu ya Sekretarieti hiyo yaliyopo Accra, nchini Ghana.

Pamoja na mambo mengine yaliyojiri katika mazungumzo hayo, Prof. Kahyarara alimpongeza Mhe. Wamkele kwa hatua nzuri iliyofikiwa katika utekelezaji wa Mkataba wa AfCFTA na kusisitiza utayari wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuendelea kushiriki kikamilifu katika kutekeleza Mkataba huo.

Naye Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya AfCFTA Mhe. Wamkele Mene aliipongeza Tanzania kwa kuwasilisha Hati ya kuridhia mkataba wa AfCFTA kwenye Kamisheni ya Umoja wa Afrika na kuwa nchi ya 40 kati ya nchi 55 za Afrika kufanya hivyo na alitoa wito kwa Watanzania wenye vigezo stahiki kuchangamkia fursa za kazi zinazoendelea kutangazwa na Sekretarieti ya AfCFTA.

Aidha , Viongozi hao walikubaliana kuendelea kushirikiana katika masuala yanayohusu Mtangamano wa Afrika kupitia Mkataba wa AfCFTA hususani katika kukuza uwekezaji katika Sekta ya Usafirishaji na Uwezeshaji Biashara, Uongezaji thamani mazao ya kilimo na  uzalishaji madawa

Katibu Mkuu, Prof. Godius Kahyarara yupo nchini Ghana kushiriki Mkutano wa 10 wa Maafisa Waandamizi wa Biashara wa Afrika unaofanyika Accra, Ghana kuanzia tarehe 24-27 Januari 2022. Mkutano huo utafuatiwa na Mkutano wa Nane (8) wa Baraza la Mawaziri wa Biashara wa Afrika utakaofanyika kuanzia tarehe 28-29 Januari 2022.

Prof. Godius Kahyarara, Katibu Mkuu, Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara (Kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Wamkele Mene, Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA).



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Tanzania Itaendelea Kushiriki Kikamilifu Kutekeleza Mkataba Wa AfCFTA
Tanzania Itaendelea Kushiriki Kikamilifu Kutekeleza Mkataba Wa AfCFTA
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEjNa52NBVAk5du20x_Bb746ejB38W920rlUEAJPEKrlOJhkYiVI6nSe1KEVdPfOjv2Yk2m-aP7vbfxUyFgrPrsSFe7kEFiGUDq5lAWJFMMYzshfDPfFdsVHcP-Jj12nQU_9fxm-Wtu2GYcud1b56__-4qlgRXvPa7g3sQP4qdjn_IPpu4VsEWGKxA3jww=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEjNa52NBVAk5du20x_Bb746ejB38W920rlUEAJPEKrlOJhkYiVI6nSe1KEVdPfOjv2Yk2m-aP7vbfxUyFgrPrsSFe7kEFiGUDq5lAWJFMMYzshfDPfFdsVHcP-Jj12nQU_9fxm-Wtu2GYcud1b56__-4qlgRXvPa7g3sQP4qdjn_IPpu4VsEWGKxA3jww=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/01/tanzania-itaendelea-kushiriki.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/01/tanzania-itaendelea-kushiriki.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy