Rais Samia Kuwapa kazi mpya William Lukuvi, Palamagamba Kabudi
HomeHabari

Rais Samia Kuwapa kazi mpya William Lukuvi, Palamagamba Kabudi

Rais Samia Suluhu Hassan ametolea ufafanuzi kuhusu viongozi wawili walioachwa katika baraza jipya la mawaziri lililotangazwa Jumamosi Jan...


Rais Samia Suluhu Hassan ametolea ufafanuzi kuhusu viongozi wawili walioachwa katika baraza jipya la mawaziri lililotangazwa Jumamosi Janauri 08, 2022 huku akisema amewapangia kazi maalumu.

Ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Januari 10, 2022 katika hafla ya uapisho wa viongozi mbalimbali walioteuliwa hivi karibuni ambapo amewataja viongozi hao wawili aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi na aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi.

“Nina kaka zangu wawili, William Lukuvi na Palamagamba Kabudi ukiwatazama hao umri wao ni kama wangu na niliowateua hamfanani kabisa kwahiyo kaka zangu hawa nimewavuta waje kwangu ili waje wanisimamie kuwasimamia nyie kwahiyo kuwaacha kwangu kwenye ile orodha hapo wote ni wadogo na mnahitaji kusimamiwa vizuri.

 “Kaka yangu Kabudi amefanya kazi nzuri sana kusimamia mazungumzo ya Serikali na mashirika na ndiyo kazi ninayotaka nimkabidhi sasa kindakindaki aendelee na kazi hiyo ila kazi yake kwasababu haipo kwenye muundo haitangazwi, mashirika yote kazi zote zitakazoingia ubia na Seriikali yeye ataongoza hiyo timu kwahiyo yeye ni baba mikataba,” amesema Rais Samia Suluhu Hassan

Rais Samia amewataka baadhi ya viongozi na Watanzania kwa ujumla kuacha kumchafua aliyekua Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akisema kuwa waziri huyo ameitumikia nchi kwa uadilifu mkubwa.

Rais Samia ameweka wazi kuwa Lukuvi hana mpango wa kugombea nafasi ya uspika kama wengine wanavyodhani.

“Kaka yangu Lukuvi yeye ana kazi na mimi mtaisikia baadae lakini ninamvuta Ikulu kazi yetu ni kuwasimamia nyie, kwasababu nikiwatamazama hapo wote wanakaribia kustaafu bado miaka miwili wengine mna safari ndefu mimi na wale tulishastaafu kwahiyo kazi yetu sasa ni kushika kiboko kuwasimamia nyie na makatibu wakuu.

“Nimeona meseji nyingi wengine wanasema afadhali Lukuvi katoka, hajatoka yupo, wengine wameanza kumletea meseji za ajabu wakijua atagombania uspika, hatagombania ana kazi na mimi msianze kumchafua ametumikia taifa hili kwa uadilifu kwa muda mrefu muacheni aende na mimi ,” amesema Rais.



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Rais Samia Kuwapa kazi mpya William Lukuvi, Palamagamba Kabudi
Rais Samia Kuwapa kazi mpya William Lukuvi, Palamagamba Kabudi
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEjB7HLYMDqOX1cIRDvm40fIw6SG_HIH6f8zIQOcGF7ZkwBrPUusaSCk5MddsBjhpW9NyJH_eGj66YKENj3ZQlJFy7XLlzIeGtVnkUeF0cN-NZ_rASM5c7HSOu5sd7vfzavM8QM2607Ydb4B4kVdfxYJWwHD9RADXYHn16hyrLDimnnYoR3yNBT7C7aaJg=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEjB7HLYMDqOX1cIRDvm40fIw6SG_HIH6f8zIQOcGF7ZkwBrPUusaSCk5MddsBjhpW9NyJH_eGj66YKENj3ZQlJFy7XLlzIeGtVnkUeF0cN-NZ_rASM5c7HSOu5sd7vfzavM8QM2607Ydb4B4kVdfxYJWwHD9RADXYHn16hyrLDimnnYoR3yNBT7C7aaJg=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/01/rais-samia-kuwapa-kazi-mpya-william.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/01/rais-samia-kuwapa-kazi-mpya-william.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy