Jafo Asitisha Shughuli Za Uchimbaji Wa Madini Ya Nickel Mlima Yobo Wilayani Chamwino
HomeHabari

Jafo Asitisha Shughuli Za Uchimbaji Wa Madini Ya Nickel Mlima Yobo Wilayani Chamwino

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo amesitisha shughuli za uchimbaji wa madini ya nic...


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo amesitisha shughuli za uchimbaji wa madini ya nickel katika eneo la mlima wa Yobo wilayani Chamwino mkoani Dodoma kutokana na kutokidhi Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004.

Ametoa maelekezo hayo Desemba 30, 2021 wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya  kutembelea na kukagua shughuli za mazingira katika maeneo ya wachimbaji wilayani humo

Dkt. Jafo alimtaka mwekezaji huyo wa kuusajili mradi huo katika ofisi za Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Kanda ya Kati ili wataalamu wajiridhishe kuhusu athari za mazingira katika eneo hilo.

“Hawa watu huko chini wataathrika na athari zinazoweza kutokea kutokana na uchimbaji huu usiofuata matakwa ya sheria na baadaye watakuja kuilaumu Serikali kwa hiyo namuagiza aanze mara moja mchakato wa kupata Cheti cha Athari kwa Mazingira (EIA),” alisema Dkt. Jafo.

Alisema pamoja na kwamba wachimbaji wengi wanadai wana mpango kazi wa kulinda mazingira lakini hauwezi kukidhi matakwa ya Sheria ya Usimamizi wa Mazingira yam waka 2004 hivyo wanawajibika kupata EIA.

Aidha, Waziri Dkt. Jafo alisisitiza kuwa ni kweli tunajenga uchumi hususan katika sekta ya uchimbaji wa madini mbalimbali nchini lakini ni lazima uendane na uhifadhi wa mazingira.

Katika hatua nyingine Waziri huyo akiwa wilayani humo alifanya ziara katika eneo linalochimbwa madini aina ya graphite lililopo Kijiji cha Itiso na kubaini uchimbaji wa mashimo usiofuata taratibu.

Kautokana na hali hiyo alitoa miezi sita kwa Kampuni ya China Dragon inayofanya shughuli hizo hapo kuhakikisha wanakarabati eneo hilo ikiwemo kufukia mashimo hayo ili kukidhi matakwa ya mazingira.

Pia alitoa mwezi mmoja kwa kampuni kuja na mpango kazi wa namna gani watatekeleza maelezo hayo huku akiiagiza NEMC Kanda ya Kati kumpa taarifa ya utekelezaji wa agizo ndani ya kipindi hicho.


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Jafo Asitisha Shughuli Za Uchimbaji Wa Madini Ya Nickel Mlima Yobo Wilayani Chamwino
Jafo Asitisha Shughuli Za Uchimbaji Wa Madini Ya Nickel Mlima Yobo Wilayani Chamwino
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEiWztTs78ZolEaH7HFmHVVZXmmugD_TLus8dBQG8IcwvdYD5VteBkljmfbPMlbUfV2hNTUjSS6ESfSiMJaFL96kWo5vKNSauEzTP8EJcmK_XAHB5sgOEd74qTF3_kBXj8M0CphUqUU3hqDVLhp8ADG76kG0dart5uHah949MW0xZEfz1v2xmh_oQ5KOfw=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEiWztTs78ZolEaH7HFmHVVZXmmugD_TLus8dBQG8IcwvdYD5VteBkljmfbPMlbUfV2hNTUjSS6ESfSiMJaFL96kWo5vKNSauEzTP8EJcmK_XAHB5sgOEd74qTF3_kBXj8M0CphUqUU3hqDVLhp8ADG76kG0dart5uHah949MW0xZEfz1v2xmh_oQ5KOfw=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/12/jafo-asitisha-shughuli-za-uchimbaji-wa.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/12/jafo-asitisha-shughuli-za-uchimbaji-wa.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy