Waziri Mkuu: Bilioni 1.6 Kuchagiza Taifa Stars Kufuzu Kombe La Dunia Qatar 2022
HomeHabari

Waziri Mkuu: Bilioni 1.6 Kuchagiza Taifa Stars Kufuzu Kombe La Dunia Qatar 2022

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa wito kwa Watanzania pamoja na wadau wa soka nchini kuungana kwa pamoja na kuhakikisha timu ya Taifa ya...


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa wito kwa Watanzania pamoja na wadau wa soka nchini kuungana kwa pamoja na kuhakikisha timu ya Taifa ya Tanzania ya mpira wa Miguu (Taifa Stars) inafanya vizuri kwenye michezo yote iliyobaki ili kufuzu kushiriki kombe la Dunia litakalofanyika nchini Qatar 2022.

Ametoa wito huo leo (Alhamis, Novemba 4, 2021) wakati akiongoza Kikao cha pamoja cha wadau wa soka Nchini katika ukumbi wa uwanja wa Taifa wa Uhuru, jijini Dar es Salaam. Ambapo katika kikao hicho wadau wa Taifa Star wamechangia Shilingi Bilioni 1.6 ambazo zitatumika kuihudumia timu katika maandalizi ya mechi zilizobaki za kufuzu kombe la Dunia.

Akizungumza kwenye kikao hicho, Mheshimiwa Majaliwa amesema ni lengo la Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha anakuza sekta ya michezo nchini na anataka kuona mafanikio katika timu za Taifa hivyo mikakati ya kuifanya timu ya Taifa ifanikiwe ni sehemu ya kutimiza malengo ya Mheshimiwa Rais.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu ametoa wito kwa wamiliki wa viwanda, Taasisi za Umma na binafsi pamoja na wadau wengine kuendelea kujitokeza kuichangia timu ya Taifa ili iweze kuweka Historia ya kushiriki kombe la dunia kwa mara ya kwanza.

Wadau Walioshiriki katika kikao hicho ni pamoja na GSM, TAIFA GAS, AZAM, CRDB, NBC, LAKE OIL, STAR OIL, K4 SECURITY, KAMBIASO pamoja na wadau wengine.

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Waziri Mkuu: Bilioni 1.6 Kuchagiza Taifa Stars Kufuzu Kombe La Dunia Qatar 2022
Waziri Mkuu: Bilioni 1.6 Kuchagiza Taifa Stars Kufuzu Kombe La Dunia Qatar 2022
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEglIAJ2hgEMP02NOwUpWpKE5YiEohJU-F1-S6pcQoByB1klN5uNfOZVONie5g8p5-g1lKn7HBW9mqCis9d8pBotxO8aPmfRcAJxC31bddoDMVbPZ225_Ta70uTX0YOgSbbvtTqWGBMiwyNV9KNzUGBabmJHb9Wvz2FHNOvLuarVG9QEOqMG_tk8TvsXOg=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEglIAJ2hgEMP02NOwUpWpKE5YiEohJU-F1-S6pcQoByB1klN5uNfOZVONie5g8p5-g1lKn7HBW9mqCis9d8pBotxO8aPmfRcAJxC31bddoDMVbPZ225_Ta70uTX0YOgSbbvtTqWGBMiwyNV9KNzUGBabmJHb9Wvz2FHNOvLuarVG9QEOqMG_tk8TvsXOg=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/11/waziri-mkuu-bilioni-16-kuchagiza-taifa.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/11/waziri-mkuu-bilioni-16-kuchagiza-taifa.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy