Mwigulu Nchemba: Tanzania ina mabilionea 5,740
HomeHabari

Mwigulu Nchemba: Tanzania ina mabilionea 5,740

Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk. Mwigulu Nchemba amesema Tanzania ina jumla ya mabilionea 5,740 sawa na asilimia 4.2 ya utajiri katika kund...

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Disemba 18
Rais Samia Aongoza Kikao Cha Kamati Kuu Ya Halmashauri Kuu Taifa Ya CCM Dodoma
Freeman Mbowe na Wenzake Wagonga Mwamba Mahakamani


Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk. Mwigulu Nchemba amesema Tanzania ina jumla ya mabilionea 5,740 sawa na asilimia 4.2 ya utajiri katika kundi la mabilionea 140,000 waliopo Barani Afrika.

Dk. Mwigulu ametoa kauli hiyo leo tarehe 4 Novemba, 2021 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Mlalo, Rashid Abdallah Shangazi (CCM).

Shangazi amehoji Tanzania ina idadi ya watu takribani milioni 55 wenye madaraja tofauti ya uchumi; Je, katika idadi hiyo Tanzania ina mabilionea wangapi?

Akijibu swali hilo, Nchemba amesema kutokana na utafiti uliofanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mwaka 2014/2015 na kurejewa mwaka 2019/2020, unaonesha idadi ya mabilionea duniani inakadiriwa kufikia watu milioni 14.

“Na kwa mujibu wa ya report ya RBC Wealth management ya Julai mwaka 2019, bara la Afrika lina mabilionea 140,000 sawa na asilimia moja ya mabilionea wote duniani,” amesema.

Amesema miongoni mwa mabilionea 5,740, waliopo Tanzania, mabilionea 115 sawa na asilimia mbili ya utajiri wa dola za Marekani milioni 30, wanamiliki zaidi ya asilimia 28 ya utajiri wote wa mabilionea wanaotoka Tanzania.

“Kati ya hawa wengi wamesajiliwa TRA, na wanalipa kodi zao katika idara ya walipa kodi wakubwa. Na wamewekeza katika sekta ya viwanda, nishati, madini na wamewekza pia katika sekta ya fedha, mawasiliano, uchukuzi, utalii na makazi,” amesema.

Aidha, amesema mabionea hao wanatoka katika sekta mbalimbali kama vile madini, viwanda, mawasiliano na ujenzi na sekta nyingine ambazo hakuzitaja .




Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Mwigulu Nchemba: Tanzania ina mabilionea 5,740
Mwigulu Nchemba: Tanzania ina mabilionea 5,740
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEisBXj-tYgsJ8BEmwdOeGChI5LjHUsOXSiwk98c208aR0rjWUNgCug2ucdhj9xle1fzUb2ljfOJadDVorC14-aU8Vc3del3vbTOSE895uFnQi3abzNd8zBhqkm8Bw6yV9IVkAewaYDRTI1fuI73xGOCxBVpcVvMH7tSuknkeIVppjB2zuOsNSVpMU8nKw=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEisBXj-tYgsJ8BEmwdOeGChI5LjHUsOXSiwk98c208aR0rjWUNgCug2ucdhj9xle1fzUb2ljfOJadDVorC14-aU8Vc3del3vbTOSE895uFnQi3abzNd8zBhqkm8Bw6yV9IVkAewaYDRTI1fuI73xGOCxBVpcVvMH7tSuknkeIVppjB2zuOsNSVpMU8nKw=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/11/mwigulu-nchemba-tanzania-ina-mabilionea.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/11/mwigulu-nchemba-tanzania-ina-mabilionea.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy