Waziri Gwajima aitaka Diaspora Urusi kuchangamkia fursa Tanzania
HomeHabari

Waziri Gwajima aitaka Diaspora Urusi kuchangamkia fursa Tanzania

 Na.WAMJW Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima amewataka Watanzania wanaoishi na kusoma nchini...

 Na.WAMJW
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima amewataka Watanzania wanaoishi na kusoma nchini Urusi kutumia fursa zilizopo Tanzania katika kuwekeza na kuwasaidia Watanzania.

Dkt. Gwajima ameyasema hayo jijini Saint Petersburg nchini hapa alipokutana ma kufanya mazungumzo na Watanzania wanaoishi na wanaosoma katika Vyuo mbalimbali.


Waziri Dkt. Gwajima amesema kuwa Tanzania ina fursa nyingi za kuwekeza katika Sekta mbalimbali katika kusaidia jamii ikiwemo Sekta ya Afya, Utalii na Madini ambazo zinaweza kuchangia katika Maendeleo ya Taifa.

Ameongeza kuwa kuishi au kusoma nje ya Tanzania hakufungi milango kuwekeza nyumbani na kuleta mabadiliko katika Taifa ulilotoka ila ndio linaongeza fursa na nafasi ya kuleta mabadiliko katika jamii kutokana na mambo mapya ya kujifunza kutoka Mataifa mengine.

"Niwaambie ndugu zangu nyumbani kumenoga wekezeni nyumbani haijalishi wewe unaishi huku au wewe ni mwanafunzi mnaweza mkajiunga pamoja na kuanzisha umoja wenu mkatafuta wafadhili mkiwa Urusi na mkawasaidia Watanzania wenzenu"  alisema Waziri Dkt. Gwajima

Aidha, amesisitiza kuwa Serikali ya Tanzania ipo pamoja na Watanzania wanaoishi na kusoma nje ya Tanzania kwani azma ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imeweka mazingira rafiki katika kuhakikisha wanapata fursa za kuchangia katika maendeleo ya Taifa huko huko walipo ikiwemo kuwekeza katika Sekta mbalimbali nchini.

Kwa upande wake Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Urusi Dkt.Switbert Mkama amemuhakikishia Waziri Dkt.Gwajima kushirikiana na Watanzania wanaoishi na kusoma nchini humo kuweza kupata fursa zilizopo Tanzania katika kuwekeza na kusaidia jamii katika Sekta mbalimbali.

"Mhe. Waziri tutawashika mkono hawa wenzetu huku na kuwapa taarifa za fursa zilizopo nyumbani ili waweze kutoa mchango wao katika maendeleo ya Taifa letu hata wakiwa nje ya Tanzania" alisema Mhe. Mkama

Naye,Mkurugenzi wa Idara ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na Msajili wa NGOs nchini Vickness Mayao amesema inawezekana kwa Watanzania wanaoishi na kusoma nje kuweza kujipanga na kufungua NGO nchini kwani taratibu zinaruhusu kuanzishwa kwa NGOs za Kimataifa nchini na kuwataka kuchangamkia fursa hiyo katika kuhakikisha wanatumika fursa walinazopata kuwa nje ya Tanzania kusaidia jamii.

Akizungumza kwa niaba ya Watanzania wanaoishi na kusoma nchini Urusi Lucas Muchunguzi ameishukuru Serikali ya Tanzania chini ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwawezesha Watanzania kupata fursa za kusoma nje ya nchi na wameaahidi kutumia uzoefu na elimu watakayoipata kusaidia kuleta mabadiliko na kichangi katika maendeleo ya Taifa



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Waziri Gwajima aitaka Diaspora Urusi kuchangamkia fursa Tanzania
Waziri Gwajima aitaka Diaspora Urusi kuchangamkia fursa Tanzania
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEiNOSfsdrChnnfnLsIBeBD_hr0oyzLmA4h8Q0baka8rz2c6A037TzqfdtA54viqYXC-rpbNxh39YE2CerS4a2M6QijvOi1i-mtVO7P1SzNQBo3uJVr6X3eD1TDkMypGuCAI5npJD6YT8B218R6z7mD_3YHeqT6Dqdq89qnmg2P05106BTuWkWqpY60WMg
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEiNOSfsdrChnnfnLsIBeBD_hr0oyzLmA4h8Q0baka8rz2c6A037TzqfdtA54viqYXC-rpbNxh39YE2CerS4a2M6QijvOi1i-mtVO7P1SzNQBo3uJVr6X3eD1TDkMypGuCAI5npJD6YT8B218R6z7mD_3YHeqT6Dqdq89qnmg2P05106BTuWkWqpY60WMg=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/10/waziri-gwajima-aitaka-diaspora-urusi.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/10/waziri-gwajima-aitaka-diaspora-urusi.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy