KUREJEA KWA TONOMBE MUKOKO KWAIPA UGUMU YANGA
HomeMichezo

KUREJEA KWA TONOMBE MUKOKO KWAIPA UGUMU YANGA

 KUREJEA kwa kiungo mkabaji, Mkongomani  Mukoko Tonombe kumelipa ugumu benchi la  ufundi la timu hiyo linaloongozwa na Mtunisia  Nasreddin...

VIDEO:TAMBO ZA MZEE WA MAJENEZA, AZUNGUMZIA ISHU YA HAJI MANARA
SIMULIZI YA MUME ALIYEKUWA AKIPIGWA NA MKEWE KILA WAKATI
REAL MADRID WABISHI, WAWEKA MKWANJA WA MAANA KUIPATA SAINI YA MBAPPE

 KUREJEA kwa kiungo mkabaji, Mkongomani 
Mukoko Tonombe kumelipa ugumu benchi la ufundi la timu hiyo linaloongozwa na Mtunisia Nasreddine Nabi na msaidizi wake Mrundi, Cedric Kaze.


Tonombe hajacheza mechi yoyote ya kimashindano ya Yanga msimu huu, akitumikia adhabu ya kufungiwa michezo mitatu baada ya kumpiga kiwiko mshambuliaji wa Simba, John Bocco kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC), Julai 25, mwaka huu.


Kiungo huyo mwenye hamasa katika timu hiyo akiwa uwanjani, Jumatatu aliungana na wachezaji wenzake kambini katika kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya KMC FC utakaopigwa Uwanja wa Majimaji, Songea.


Mmoja wa mabosi wa Benchi la Ufundi la Yanga, ameliambia Championi Ijumaa kuwa kurejea kwa kiungo huyo kumemfanya kocha Nabi apate ugumu wa kupanga kikosi chake cha kwanza.


Bosi huyo alisema kuwa ugumu huo anaupata kutokana na muunganiko mzuri ulikuopo kati ya viungo wawili wakongwe Khalid Aucho na Yannick Bangala ambao wamecheza michezo iliyopita na kufanya vizuri.


 Aliongeza kuwa kwa viwango ambavyo wamevionyesha katika mchezo wa Ngao ya Jamii na miwili ya ligi dhidi ya Kagera Sugar na Geita Gold, Nabi ameonekana kupata ugumu baada ya Tonombe kurejea kikosini.


“Kwa usajili bora uliofanywa na viongozi, kocha anakabiliwa na changamoto ya upangaji wa kikosi chake kutokana na ubora wa kila mchezaji.


“Ugumu umeongezeka zaidi ni baada ya kurejea kwa Tonombe ambaye alikuwa nje ya uwanja katika michezo mitatu akitumikia adhabu ya kufungiwa michezo mitatu baada ya kumpiga kiwiko Bocco.

“Tonombe anarejea uwanjani lakini tayari wapo viungo Aucho na Bangala ambao wameonekana kucheza vizuri kwa kuelewana kwa ubora mkubwa, hivyo kazi kubwa anayo Nabi,” alisema bosi huyo.

Akizungumzia hilo, Kaze alisema: “Kikubwa tuna kikosi bora na imara cha kupata matokeo mazuri, hilo ndilo jambo la kujipongeza,ushindani wa namba msimu huu ni mkubwa kutokana na ubora wa kila mchezaji. Ni kipindi chetu hivi sasa benchi la ufundi kutulia na kuandaa kikosi kitakachotupa pointi hilo ni jambo la muhimu zaidi," .



Credit: SALEH JEMBE

Please subscribe to get all sports news instantly
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: KUREJEA KWA TONOMBE MUKOKO KWAIPA UGUMU YANGA
KUREJEA KWA TONOMBE MUKOKO KWAIPA UGUMU YANGA
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEh8y6HXU6Thm6rOxhQM3rCQbSYnE9CziV_oMzL6z4cFj_7rXvhGoSUPI2K06z0iv5t6VkTc5BHh557gd2Lx0cIAPhm2Bhds3dx6y6wS3hVM-5n5z5E8UZebak13rvQ8E8IDUsdTI5Ggt5lu4Cmg6pPaQa3b-PBD8h8R1Eiv0fTO9sY-niiE3aQPD1uQRA=w640-h428
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEh8y6HXU6Thm6rOxhQM3rCQbSYnE9CziV_oMzL6z4cFj_7rXvhGoSUPI2K06z0iv5t6VkTc5BHh557gd2Lx0cIAPhm2Bhds3dx6y6wS3hVM-5n5z5E8UZebak13rvQ8E8IDUsdTI5Ggt5lu4Cmg6pPaQa3b-PBD8h8R1Eiv0fTO9sY-niiE3aQPD1uQRA=s72-w640-c-h428
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/10/kurejea-kwa-tonombe-mukoko-kwaipa-ugumu.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/10/kurejea-kwa-tonombe-mukoko-kwaipa-ugumu.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy