Baba Amuua mtoto wake kwa kumpiga na Deki Usoni kisa Matusi.
HomeHabari

Baba Amuua mtoto wake kwa kumpiga na Deki Usoni kisa Matusi.

Na John Walter-Manyara Jeshi la polisi  Mkoani Manyara linamshikilia Mkazi wa Kijiji cha Bassoutu wilayani Hanang, Elibariki Shaban kwa ...


Na John Walter-Manyara
Jeshi la polisi  Mkoani Manyara linamshikilia Mkazi wa Kijiji cha Bassoutu wilayani Hanang, Elibariki Shaban kwa tuhuma za kumpiga kwa deki usoni,  makofi na mateke mtoto wake wa kumzaa Amos Elibariki (25) na kufariki dunia akikimbizwa Hospitali.

Kamanda wa polisi Mkoani hapa Maresone Mwakyoma akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake oktoba 28,2021 alisema tukio hilo lilitokea Oktoba 26 mwaka huu majira ya saa 3:00 za usiku.

Mwakyoma alisema baba alimpiga mtoto wake huyo baada ya kubishana sana bila kutaja kitu walichokuwa wakibishania.

Alisema baba alipohojiwa na polisi sababu za kumpiga mwanae alisema alimpiga kwa kuwa mtoto huyo alimtukana na yeye hasira ilimpanda na kuamua kumuadhibu kwa kutumia deki, mateke na makofi.

Aidha alisema polisi walibaini Amos alipishana  na baba yake ndio maana baba alichukia na kuamua kumpa kichapo na baada ya kichapo alianguka chini.

Alisema Amos aliaga Dunia wakati wakimkimbiza kuelekea Hospitali ya Hydom ili apatiwe matibabu.

Katika hatua nyingine polisi wanamsikilia Mfanyakazi wa ndani Januari Makomolwa mkazi wa Kijiji cha Endagikok wilayani Mbulu kwa kumbaka mwanafunzi wa darasa la kwanza(7)  jina limehifadhiwa.

Akithibitisha tukio hilo kamanda Mwakyoma alisema lilitokea Oktoba 18 mwaka huu .

Alisema Makomolwa ambaye anafanya kazi katika familia ya mtoto huyo inadaiwa aliachiwa mtoto huyo na bosi wake ambaye ni mama wa mtoto ndipo aliamua kuanza kumfanyia unyama.

Mwakyoma alisema mama wa  mtoto aliporejea nyumbani alimkuta mfanyakazi wake akimbaka mtoto wake.

Alikiri matukio ya ubakaji kuwa mengi katika mkoa huo na akawataka wananchi wanapoajiri wafanyakazi wa ndani wahakikishe wanawachunguza kwanza.

"Tusiwaamini wafanyakazi wa ndani kwa kuwa ndugu wa karibu na marafiki wa familia ndio wanabaka watoto, "alisema Mwakyoma

Aliongeza kuwa jamii kumaliza matukio ya ubakaji kienyeji ni chanzo pia cha kuongezeka kwa ubakaji.


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Baba Amuua mtoto wake kwa kumpiga na Deki Usoni kisa Matusi.
Baba Amuua mtoto wake kwa kumpiga na Deki Usoni kisa Matusi.
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEhtk5sF5Dn6N5oqcl-_5G-y64J8K1WCouON1iCiVIi7s-xwQXINGfyN2nNxV82sYytahH2UrcY9iUyteELGHLxDFwBLj4tS6bqDTAeX91MQNnGZHc3DFnM9rjB99-hbReT4e3nv8vLRRJTzYN1fSbDW3cGdJYtaKPB1EcyCA30uRoA-aTZcPsKz-tuPtw=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEhtk5sF5Dn6N5oqcl-_5G-y64J8K1WCouON1iCiVIi7s-xwQXINGfyN2nNxV82sYytahH2UrcY9iUyteELGHLxDFwBLj4tS6bqDTAeX91MQNnGZHc3DFnM9rjB99-hbReT4e3nv8vLRRJTzYN1fSbDW3cGdJYtaKPB1EcyCA30uRoA-aTZcPsKz-tuPtw=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/10/baba-amuua-mtoto-wake-kwa-kumpiga-na.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/10/baba-amuua-mtoto-wake-kwa-kumpiga-na.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy