NYOTA watatu wa kikosi cha PSG ambao ni Lionel Messi, Neymar na Kylian Mbappe wanatarajiwa kuanza mechi moja leo kwa mara ya kwanza kwenye...
NYOTA watatu wa kikosi cha PSG ambao ni Lionel Messi, Neymar na Kylian Mbappe wanatarajiwa kuanza mechi moja leo kwa mara ya kwanza kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Nyota hao wenye uchu wa kucheka na nyavu hawajawahi kucheza pamoja tangu Messi alipotua hapo akitokea kikosi cha Barcelona.
Mashabiki pamoja na wafuatiliaji wa masuala ya mpira wanasubiri kwa shauku kujua itakuaje pacha hiyo matata.
Kocha wa PSG, Mauricio Pochettino amepanga kuwatumia wakali hao wa kucheka na nyavu kwenye mchezo wa leo dhidi ya Club Brugge ya Ubelgiji na watakuwa ugenini.
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS