MASAU BWIRE AFUNGUKA NAMNA ALIVYOPEWA OFA SIMBA, AMTAJA MANARA
HomeMichezo

MASAU BWIRE AFUNGUKA NAMNA ALIVYOPEWA OFA SIMBA, AMTAJA MANARA

  WAKATI jina la Masau Bwire, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting likitajwa kuibukia mitaa ya Msimbazi kubeba mikoba ya Haji Manara, kiongozi h...

 


WAKATI jina la Masau Bwire, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting likitajwa kuibukia mitaa ya Msimbazi kubeba mikoba ya Haji Manara, kiongozi huyo amefungukia namna mabosi wa Simba walivyompa ofa ili awe ndani ya kikosi hicho.

Kwa sasa nafasi ya Ofisa Habari wa Simba ipo mikononi mwa Ezekiel Kamwaga ambaye anakaimu nafasi hiyo na aliweka wazi kuwa atasepa hivi karibuni kwa kuwa mchakato wa kumtafuta mbadala wake unaendelea.

Akizungumza na Championi Jumatano, Masau alisema kuwa Simba walimfuata zamani ili awe kwenye kitengo cha usemaji lakini alikataa kwa kuwa roho wa Bwana hakumpa ruhusa kufanya hivyo.

 “Kuna vitu viwili unaweza kuvichanganya,kwamba mimi pengine nafurahia kwenda kufanya kazi Simba pengine ningekuwa napenda kufanya hivyo ningefanya kazi siku nyingi sana kwa sababu Simba waliwahi kunifuata ili nikafanye kazi pale.

“Simba waliwahi kunihitaji siku nyingi tena kwa nguvu lakini bado roho wa Bwana alikuwa hajaruhusu walinifuata sana nilikataa ilikuwa zama za utawala wa Aveva, (Evans) na Kaburu, (Godfrey Nyange) pengine ningekubali mimi pengine Manara, (Haji) asingekuwepo pale.


 “Walinifuatilia sana kwa kujua kwamba Hassan Hasanoo, (Othuman) alikuwa ni rafiki yangu na anaushawishi kwangu basi wakasema amesema nikamsalimie wakati huo alikuwa mahabusu  ila lengo ilikuwa ni kumtumia yeye anishawishi ili niweze kufanya kazi katika klabu hiyo nilisimamia msimamo, sio Simba tu hata Wananchi yaani Yanga walinifuata niliwaambia kwamba sipo tayari hata kipindi cha Charles Mkwasa alipokuwa katibu nilifuatwa lakini bado roho wa Bwana hakuruhusu.

“Pia Azam FC wamenifuata nakumbuka walinifuata mara tatu na kuna wakati walinifuata Uwanja wa Taifa kipindi hicho kwa sasa ni Uwanja wa Mkapa, niliwashirikisha waandishi wengine ikiwa ni pamoja na marehemu Kashasha, ila nilibaki kuwa na msimamo wangu.

“Sifurahii kwamba sasa nachukuliwa kwenda kufanya kazi huko ila furaha yangu ni namna ambavyo watu wananitazama.Sifanyi kazi kwa kufikiria kikija kitu chenyewe maamuzi yangu yatafanyika hapo.Siwezi kutoa maoni katika kitu ambacho hakipo,” alisema Masau.

 

 



Credit: SALEH JEMBE

Please subscribe to get all sports news instantly
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: MASAU BWIRE AFUNGUKA NAMNA ALIVYOPEWA OFA SIMBA, AMTAJA MANARA
MASAU BWIRE AFUNGUKA NAMNA ALIVYOPEWA OFA SIMBA, AMTAJA MANARA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgeFAj-Le0q5CAogDt6FLLEqnNjgg2zsuoAnY9a9ZI6KLNqwW8wpwbVvRP4C-Z0180AObWVqhl4PXU_MUnmLH4eAerwCSe5uJmV_Eh91cIvxkdN1q5jDQrWpojPIgoj5VgtEHpAsEmzFrwH/w640-h556/Masau+Simba.PNG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgeFAj-Le0q5CAogDt6FLLEqnNjgg2zsuoAnY9a9ZI6KLNqwW8wpwbVvRP4C-Z0180AObWVqhl4PXU_MUnmLH4eAerwCSe5uJmV_Eh91cIvxkdN1q5jDQrWpojPIgoj5VgtEHpAsEmzFrwH/s72-w640-c-h556/Masau+Simba.PNG
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/09/masau-bwire-afunguka-namna-alivyopewa.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/09/masau-bwire-afunguka-namna-alivyopewa.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy