Waziri Mkuu Aagiza Kurejeshwa Kwa Michezo Ya Shimiwi
HomeHabari

Waziri Mkuu Aagiza Kurejeshwa Kwa Michezo Ya Shimiwi

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameziagiza wizara zote zinazohusika na uratibu na uandaaji  wa Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzani...

Habari Katika Magazeti ya Leo Disemba 6
Kenya: Watu 20 wafariki dunia katika basi lililosombwa na mto
DC Mangwala Afunga Mafunzo Ya Jeshi La Akiba


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameziagiza wizara zote zinazohusika na uratibu na uandaaji  wa Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) wahakikishe wanakutana na kuweka mpango wa kurejesha michezo hiyo ili watumishi wa umma wapate fursa ya kushiriki na kujikinga na maradhi yasiyoambukiza.

Amesema michezo hiyo ya SHIMIWI ni muhimu kwa sababu ilikuwa inawakutanisha Watumishi wa Wizara za Serikali na Taasisi zake na ilisaidia sana kuboresha afya zao na kuongeza hamasa ya utendaji kazi hivyo kuongeza tija na ufanisi wa kazi.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana(Jumapili, Agosti 15, 2021) wakati alipomuwakilisha Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan wakati wa mbio za hisani za “CRDB Bank Marathon” zilizofanyika katika viwanja vya The Greens, Oysterbay  Dar es Salaam.

Waziri Mkuu amesema mashindano hayo ya SHIMIWI yaliwasaidia watumishi wa umma kupambana na magonjwa sugu yasiyoambukiza tofauti na sasa. “Nakumbuka mara ya mwisho michezo hii ilifanyika mwaka 2014.”

“…Naelekeza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kushirikiana na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jinsia, Wazee na Watoto  na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ili kuweka mikakati ya pamoja ya kufufua michezo na ushiriki wa michezo kwa watumishi, wanafunzi na wananchi kwa ujumla.”

Kadhalika, Waziri Mkuu ameiagiza TAMISEMI ihakikisheni inasimamia kwa ukaribu ushiriki wa michezo kwa watumishi na wananchi, pia michezo kama vile jogging, marathon, mchakamchaka nayo inatakiwa ipewe kipaumbele hususan kwa wanafunzi.

“Natambua kuwa Katibu Tawala wa Mkoa (RAS) na Katibu Tawala wa Wilaya (DAS) ni wenyeviti wa Kamati za Michezo za Mikoa na Wilaya katika maeneo yao.  Kwa hiyo, hakikisheni mnalisimamia jambo hilo.”

Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali kwa upande wake imeruhusu shughuli za michezo ziendelea kwa kutambua umuhimu wake katika kuimarisha afya za binadamu pamoja na kujikinga na ugonjwa wa UVIKO19. “Mazoezi kama ilivyo lishe ni muhimu sana kwenye kulinda mwili dhidi ya maradhi mbalimbali ikiwemo UVIKO19.”

Waziri Mkuu amesema kwa upande huo wa mazoezi, Shirika la Afya Duniani (WHO) linashauri watu wafanye mazoezi ya walau dakika 150 kwa wiki (yaani dk 30 kila siku kwa siku 5 za juma). “Haya ni mazoezi ya kiwango cha chini kama vile kutembea, kuendesha baiskeli.”

“Kwa msingi huo, binafsi ninafarijika sana kuona mwitikio huu mkubwa kutoka kwa Watanzania pamoja na wageni kwenye tukio hili adhimu. Kwa lugha nyingine, ushiriki wenu kwenye mbio hizi za CRDB Bank Marathon ni kielelezo tosha kuhusu utayari na utu mlionao katika kuchangia watoto wetu kupata huduma za upasuaji wa moyo.”

Amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango huo katika kuwapunguzia mzigo wazazi na walezi wa watoto hawa. “Nyote mtakubaliana nami kuwa kuuguza si jambo la lelemama hasa unapouguza mtoto. Jambo la kuuguza mtoto husababisha wasiwasi na maumivu kwa wazazi na walezi hasa tunapokuwa tukishuhudia watoto wetu wakiugulia maumivu ya ugonjwa.”

“Nimefahamishwa kuwa ushiriki wenu kwenye mbio hizi, utawezesha upatikanaji wa fedha za kuanzisha Kituo cha Taarifa za Saratani (Cancer Information Centre) katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road.  Kituo hiki kitakuwa kiungo muhimu kati ya wagonjwa wa saratani, wanaohudumia wagonjwa wa saratani na wale wenye wasiwasi juu ya saratani.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela alisema hii ni mara ya pili kwa benki hiyo kuandaa mbio hizo, Agosti mwaka jana ambapo zaidi ya watu 4,000 walichangia watoto 100 kupata tiba ya upasuaji wa moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa gharama ya shilingi milioni 200.

Alisema lengo la mbio za mwaka huu ni kuendelea kushirikiana na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na kuanzisha Kituo cha Taarifa za Saratani (Cancer Information Centre) katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road pamoja na kuimarisha afya zao kwa kufanya mazoezi huku wakijumuika na familia, rafiki na jamii.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Waziri Mkuu Aagiza Kurejeshwa Kwa Michezo Ya Shimiwi
Waziri Mkuu Aagiza Kurejeshwa Kwa Michezo Ya Shimiwi
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjsF5ZIs5TU-ih2AXyUyVrOT4cc-rOJzHPGExDetsu3udvAY8MkRSRvjMwIs7dQo8-1uCYwsYabHDnzyAslLWaQB4vG2rw2dXnRxwxxcos1BTBm2DB3PxwhN6e1J3vaNtfk8FlyAymhsKRL/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjsF5ZIs5TU-ih2AXyUyVrOT4cc-rOJzHPGExDetsu3udvAY8MkRSRvjMwIs7dQo8-1uCYwsYabHDnzyAslLWaQB4vG2rw2dXnRxwxxcos1BTBm2DB3PxwhN6e1J3vaNtfk8FlyAymhsKRL/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/08/waziri-mkuu-aagiza-kurejeshwa-kwa.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/08/waziri-mkuu-aagiza-kurejeshwa-kwa.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy