Serikali Kupeleka Chanjo Ya Corona Makambi Ya Wakimbizi
HomeHabari

Serikali Kupeleka Chanjo Ya Corona Makambi Ya Wakimbizi

 Na Abubakari Akida,MOHA Serikali imesema iko katika mpango wa kupeleka Chanjo ya UVIKO 19 katika Makambi na Makazi ya Wakimbizi katika mi...

 Na Abubakari Akida,MOHA
Serikali imesema iko katika mpango wa kupeleka Chanjo ya UVIKO 19 katika Makambi na Makazi ya Wakimbizi katika mikoa ya Kigoma,Tabora na Katavi ikiwa ni mpango mkakati wa kukabiliana na wimbi la tatu la ugonjwa huo.

Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Khamis Hamza Chilo wakati alipotembelea Kituo cha Afya cha Katumba kinachotumiwa na wakimbizi na raia wapya wanaokadiriwa kufikia 86,233  toka nchini Burundi ambao walikimbia mapigano ya kikabila yaliyotokea nchini kwao 1974.


“Katika kukabiliana na janga la UVIKO 19 tayari Wakuu wa Makambi washaanza  kutambua idadi ya watu ambao wanauhitaji wa hiari wa kupata chanjo hiyo ili jamii ya wakimbizi wanaokaa katika makambi yaliyopo nchini ili muda ukifika tuwe na takwimu sahihi za wanaohitaji kuchanjwa na tayari kama mnavyoona tayari zoezi la chanjo lishaanza baada ya siku chache kuzinduliwa na Rais Mama Samia Suluhu Hassan na viongozi mbalimbali wa ngazi za juu,wito pekee naotoa kwa wakimbizi kufuata ushauri wa wataalamu wa afya katika kujikinga na maradhi hayo ambayo dunia sasa inapitia” amesema Naibu Waziri Chilo

Akizungumzia idadi ya wagonjwa wa UVIKO 19 katika Kituo cha Afya Katumba, Mganga Mfawidhi wa kituo hicho,Dkt.Veneranda Msati amesema hawana mgonjwa aliyefika kituoni huku akielezea utolewaji wa elimu ya kujikinga na ugonjwa huo kwa wagonjwa na mama wajawazito wanaofika katika kituo hicho kupata huduma.

“Kwasasa katika kituo chetu hatuna mgonjwa yoyote wa Corona tunachofanya ni kutoa ushauri wa kujikinga na maradhi hayo kwa wagonjwa wanaofika hapa kupata huduma za afya ikiwemo na akina mama wajawazito lakini pia tunatuma wataalamu wetu wa afya kwenda kuwafundisha wananchi katika makazi yao jinsi ya kunawa kwa maji safi tiririka na kukaa umbali unaoshauriwa ili kuepuka maambukizi ya UVIKO”amesema Dkt. Veneranda

Awali akisoma taarifa ya makazi hayo,Mkuu wa Makazi ya Katumba,John Mwita amesema hali ya usalama ni shwari huku wakiendelea kutoa elimu na kufuata sheria za kuishi katika makazi kwa wakimbizi hao.

BONYEZA HAPA KUJUA VITUO VITAKAVYOTOA CHANJO YA CORONA TANZANIA



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Serikali Kupeleka Chanjo Ya Corona Makambi Ya Wakimbizi
Serikali Kupeleka Chanjo Ya Corona Makambi Ya Wakimbizi
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiMf_oS-mMZ_H1H7gf59LVZ0rY_cVxPyp1XwPnabVWVhAuc9UhbUduQMZwUkMrQRX8bbzq5z2Ls7R-LS8FzOlEPgw8-dNWTT0zeu29msJXwcLoAceqVYLQuE98xXVk4l91Tjml4MFJ44sKA/s0/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiMf_oS-mMZ_H1H7gf59LVZ0rY_cVxPyp1XwPnabVWVhAuc9UhbUduQMZwUkMrQRX8bbzq5z2Ls7R-LS8FzOlEPgw8-dNWTT0zeu29msJXwcLoAceqVYLQuE98xXVk4l91Tjml4MFJ44sKA/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/08/serikali-kupeleka-chanjo-ya-corona.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/08/serikali-kupeleka-chanjo-ya-corona.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy