Naibu Waziri Mabula Ataka Wadau Kushirikishwa Utekelezaji Mpango Kabambe
HomeHabari

Naibu Waziri Mabula Ataka Wadau Kushirikishwa Utekelezaji Mpango Kabambe

Na Munir Shemweta, MANYARA Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amezitaka Halmashauri zote nchini kuh...


Na Munir Shemweta, MANYARA
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amezitaka Halmashauri zote nchini kuhakikisha zinashirikisha wadau wa sekta mbalimbali wakati wa utekelezaji Mpango Kabambe katika maeneo yao.

Aidha, alitaka mipango kina inayoandaliwa katika halmashauri za Miji na Majiji kuhakikisha inazingatia mipango kabambe inayoandaliwa ili kuifanya miji kuwa na taswira nzuri.

Dkt Mabula alieleza hayo jana tarehe 12 Agosti 2021 wilayani Babati mkoa wa Manyara wakati akizindua Mpango Kabambe wa Mji wa Babati akiwa katika ziara yake ya siku moja ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi katika mkoa wa Manyara.

Alisema, ni vizuri watendaji wa halmashauri kuhakikisha wakati wa utekelezaji mipango kabambe wanashirikisha wadau kama vile sekta za maji, barabara na umeme na kusisitiza kuwa hawatakiwi kwenda kinyume na yaliyowekwa katika mpango huo ili kuifanya miji kuwa na taswira nzuri na inayovutia.

Naibu Waziri wa Ardhi aliongeza kwa kusema kuwa, Wizara yake inaendelea kuhamasisha uandaaji mipango kabambe kwenye maeneo mengine nchini ili kuongeza kasi ya upimaji pamoja na kuifanya miji kuwa katika sura nzuri.

“Kikubwa utekelezaji uzingatie mpango na lazima uwekwe wazi kwa kushirikisha wadau na kumkabidhi kila mdau kipande chake cha utekelezaji mfano barabara TANROAD au TARURA akabidhiwe, umeme TANESCO na maji wapewe mamlaka ya maji na utekelezaji uzingatie mpango usiende kinyume” alisema Dkt Mabula

“Unakuta barabra nzuri halafu anakuja mtu wa maji anapitisha mabomba yake na anaharibu kabisa na hapa lengo ni kuona miji yote inapangwa vizuri” Naibu Waziri Mabula.

Aidha, Dkt Mabula aliuelezea mpango kabambe aliouzindua kama njia mojawapo ya kutoa fursa za ajira sambamba na kuongeza kasi ya upimaji na hivyo kupunguza ama kuondoa migogoro ya ardhi.

Alizitaka Halmashauri ambazo bado hazijandaa mipango kabambe kuiga mfano wa halmashauri ya mji wa Babati kwa kuandaa mipango kabambe ili kuchangia shughuli za kiuchumi na kuagiza ofisi za mikoa na wilaya kufuatilia na kupatiwa ripoti ya utekelezaji Mpango Kabambe katika halmashauri husika ili kuleta maendeleo ya kichumi na kimazingira.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Makazi Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi. Imaculata Senje alisema lengo la serikali katika uandaaji mpango kabambe ni kuona kasi ya upangaji inaoongezeka.

Kwa mujibu wa Bi. Senje, hadi sasa jumla ya mipango Kabambe 30 imeandaliwa kwenye makao makuu ya wilaya nchini na kusisitiza kuwa mipango hiyo inapoandaliwa hushirikisha sekta zote muhimu kama vile barabara, maji, umeme nk.

“Mipango unapoandaliwa inazingatia miradi ya kutekelezwa inayogusa sekta zote na ndiyo maana wakati wa uandaaji tunashirikisha sekta zote na gharama zinazoainishwa katika mpango ni kwa ajili ya miaka ishirini .


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Naibu Waziri Mabula Ataka Wadau Kushirikishwa Utekelezaji Mpango Kabambe
Naibu Waziri Mabula Ataka Wadau Kushirikishwa Utekelezaji Mpango Kabambe
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhntbOMB-4y6llTyuhSd7AtN-kEd_nTUddFi8uQM1KCJO5Npas5phtdIIT4ApiupmY0DnGtP6YM-OOkWv9CGw9FUvyWZ_J55P2noV2k56ObZv_b3L8GBz0hzIm8H8Rl4MUm31YNp3M6b3GA/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhntbOMB-4y6llTyuhSd7AtN-kEd_nTUddFi8uQM1KCJO5Npas5phtdIIT4ApiupmY0DnGtP6YM-OOkWv9CGw9FUvyWZ_J55P2noV2k56ObZv_b3L8GBz0hzIm8H8Rl4MUm31YNp3M6b3GA/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/08/naibu-waziri-mabula-ataka-wadau.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/08/naibu-waziri-mabula-ataka-wadau.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy