K OCHA Msaidizi wa AS Vita, Raoul Shungu ameibuka na kusema kuwa kitendo cha Yanga kuwanasa nyota wake wawili, mshambuliaji Fiston M...
KOCHA Msaidizi wa AS Vita, Raoul Shungu ameibuka na kusema kuwa kitendo cha Yanga kuwanasa nyota wake wawili, mshambuliaji Fiston Mayele na beki Djuma Shaban basi ana uhakika wapinzani wao wakiwemo Simba watapata tabu kutokana na kuutambua ubora wa wachezaji hao.
Shungu ametoa kauli hiyo baada ya Yanga kumalizana na nyota hao wa AS Vita kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Shungu alisema kuwa kwake Mayele na Djuma ni wachezaji wakubwa na wenye uzoefu wa michuano mikubwa, hivyo anaamini watakuwa na mchango wa kutosha ndani ya Yanga katika msimu ujao wa ligi.
“Kiukweli sina shida ya ubora wa Djuma wala Mayele kwa sababu ni wachezaji wenye uzoefu mkubwa na michuano ya kimataifa na wana uwezo wa kucheza kwenye uwanja wowote kama ilivyokuwa kwa Mukoko (Tonombe) na Tuisila (Kisinda) ambavyo wamefanikiwa katika ligi ya huko.
"Naamini timu pinzani watapata tabu kutokana na namna Yanga walivyoamua kuijenga timu yao kwa sababu wanataka kuwa bora, wanataka kushinda makombe kama ilivyo kuwa huko nyuma na aina ya wachezaji wanaojaribu kuwaleta wakiwemo Mayele na Djuma,” alisema Shungu.
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS